Kampuni ya usafiri wa ndege imemlaumu abiria mmoja baada ya moja ya milango yao kudondoka punde tu walipotua.
Ndege hio iliosafiri kutoka Lagos hadi Abuja ilikuwa ikiambaa chini kwenye barabara ya kurukia ndege wakati mlango huo ukandondoka.
Kampuni hio ya Dana Air imekana kwamba chanzo cha tukio hilo kilikuwa cha kiufundi na kusema mlango huo haungeweza kudondoka " bila jitihada za maksudi za abiria aliyeufungua"
Lakini abiria mmoja ameiambia BBC kuwa kila mmoja kwenye ndege alikataa kuuchokonoa mlango huo.
Dapo Sanwo ktuoka Lagos alisema: "Safari nzima ilikuwa ya kelele na mitetemo kutoka sakafu. Niliona kitasa cha mlango wa dharura kilikuwa kimelegea na kuning'inia."
"Tulipotua na ndege ikaanza kuambaa chini , tulisikia mlipuko mdogo, na wimbi mkubwa wa upepo na kelele. Ilikuwa mbaya sana."
"Wahudumu wa ndege walijaribu kumsingizia abiria kuwa alivuta kitasa lakini kila mmoja alikataa. Walijaribu pia kutuzuia kuchukua video na picha"

Katika taarifa iliotolewa na Dana Air, kampuni hio imekanusha kuwa na hitilafu yoyote katika safari nzima
"Mlango wetu wa dharura zimefungwa kikamilifu na hauwezi kudondoka bila mtu kuuchokonoa au kujaribu kwa maksudi kufunguliwa na mfanyakazi wa ndege au abiria," kampuni hio imesema.
" Wakati ndege ipo angani, inakuwa katika mgandamizo wa juu na hamna njia ya kiti au mlango kutikisika kama inavyosemwa"
Kampuni iliendela kusema kuwa ndege ilikaguliwa na wahandisi pamoja na Mamlaka ya Usafirishaji wa Anga Nigeria na "hamna hitilafu iliyoripotiwa"
Mwaka 2012, ndege ya Dana Air ilianguka kwenye eneo la makazi jijini Lagos na kuwauwa abiria 153.
Nigeria inahistoria ya rekodi mbaya ya usalama wa anga. Mwaka jana , uwanja wa ndege wa Abuja ulifungwa kwa wiki sita kwa ajili ya marekebisho ya barabara ya kurukia ndege
No comments:
Post a Comment