TANGAZO


Monday, February 12, 2018

Je Trump atatorokea wapi iwapo kutatokea shambulio la kinyuklia?

Trump - akisimama mbele ya nyumba yake ya Mar-a-Lago

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTrump ana handaki ndani ya nyumba yake ya Mar-a-Lago estate - lakini halina uhusiano wowote na yeye kuwa rais
Kutoka rais Truman hadi kufikia kwa Trump, Marais wa Marekani wamekuwa na mahandaki ya kukwepa mashambulio ya kinyuklia. Hivyo basi ni nini kinachofanyika iwapo kuna tisho la kinyuklia.
Mara moja rais Trump atatoroshwa katika eneo lenye usalama, ana maeneo mengi ya kumficha.
Mojawapo lipo ndani ya ikuku ya Whitehouse, handaki lililojengwa miaka 1950.
Eneo jingine liko chini ya ardhi katika eneo la Blue Ridge Mountains huko Virginia.
Pia ana handaki jingine katika nyumba yake mjini Florida na jingine ambalo hutumiwa kuhifadhi mabomu katika uwanja wake wa kucheza gofu katika eneo la West Palm Beach.
Handaki hilo linadaiwa kuwa chini ya shimo la pili katika uwanja huo.
Habari ya kumlinda Trump, iwapo kutakuwa na shambulio la bomu. inaonyesha vile Wamarekani wamekuwa walikijadili swala la kutokea kwa vita vya kinyuklia katika kipindi cha miongo kadhaa iliopita.
Kwa wengine, wazo la kuzuka kwa vita vya kinyuklia halipo katika mafikira yao. Wengine wanajiandaa.
Handaki la GreenbriarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionhandaki la Greenbrier, ambalo lilikuwa likitumiwa Congress, sasa ni kivutio cha utalii
Hathivyo hakuna handaki linaloweza kuhimili shambulio la moja kwa moja. Iwapo rais ataipuka shambulio la kwanza atalazimika kupelekwa mahali ambapo atalazimika kuliongoza taifa, hata iwapo ulimwengu uliosalia upo katika vita.
Maafisa wa Marekani wamefanya maandalizi ya rais na kundi la maafisa wa ngazi za juu serikalini , kulingana na Robert Darling ,mwanamaji aliyehudumu kipindi cha Septemba kumi na moja katika handaki la Ikulu ya Whitehouse.
Ametaja ni akina nani walioruhusiwa kuingia ndani.
Kama alivyosema Darling. Ni watu wachache pekee walioruhusiwa kuingia katika handaki la rais .
Ujenzi wa nyumba na mahandaki aidha ya marais ama raia wa kawaida una sababu yake-unafanya kuwa rahisi kwa raia wa Marekani kuzungumzia kuhusu maswala ya Atomic ama ya kinyuklia na kufanya wasio fikiriwa vita vya kinyuklia dunia kufikiria.
Harry Truman alianzisha utawala wa kiraia wa ulinzi 1950.
Ujumbe wa jumla kutoka kwa serikali ni kwamba , kulingana na Christian Appy ,muhadhiri wa somo la historia katika chuo kikuu cha Massachussets mjini Amherst, ni kwamba vita vya kinyuklia sio lazima viangamize kila mtu.
Ikuku ya White House, CIA na maafisa wa ngazi za juu wa FBI wanamsikiliza rais Bush katika handaki wakati wa shambulio la 9/11Haki miliki ya pichaUS NATIONAL ARCHIVES
Image captionIkuku ya White House, CIA na maafisa wa ngazi za juu wa FBI wanamsikiliza rais Bush katika handaki wakati wa shambulio la 9/11
Utafiti uliofanywa ulibani kwamba asilimia 30 ya waliofariki mara moja baada ya shambulio la bomu katika mji wa Nagasaki wangeokolewa iwapo wangesalia majumbani, kulingana na Sowell akielezea kuhusu mpango wa Truman wa kuwalinda raia.
Maafisa walijaribu kutengeza mfumo wa ulinzi wa kitaifa kwa wafanyika wa serikali pamoja na raia.
Maafisa walitengeza kifaa kikubwa mjini LOs Angeles , Altos, California miaka 1960 kwa mfano. Huku watu binafsi wakijenga mahandaki yao . Mmoja wao anatambulika kama Marjorie Merriweather Post, ambaye alijenga handaki lake katika eneo la Mar-a-Lago, mjini Florida.
Mapema mwaka 1950 kulikuwa na kichwa cha habari kuhusu vita vya Korea na uwezo wake wa kusambaa kwa haraka na hivyobasi akalazimika kutengeza handaki la ardhini.
Mahandaki hayo yalichimbwa chini ya ardhi na Mar-a-Lago, kulingana na idara ya maswala ya ndani nchini Marekani inayotafiti majengo ya kihistoria.
Trump alinunua jengo hilo pamoja na handaki lake 1985.
Baadaye alilitaja handaki hilo kuwa imara , likiwa limejengwa katika mwamba na vyuma na saruji. Paa lake liko chini chini kulingana na Wes Blackman.
Meneja huyo wa mradi, mwenye urefu wa futi 6 na nchi tano alilazimika kuzama wakati alipotembelea handaki hilo akiandamana na Trump miaka kadhaa iliopita.
Wes Blackman, akisimama nje
Image captionWes Blackman alitembelea handaki la Mar-a-Lago akiandamana na Trump
Ni handaki fupi na jeusi, kulingana na Blackman. Kulikuwa na nguo zilizotundikwa katika ukuta na kulikuwa na choo katikati ya chumba.
Wakati Post alipokuwa akijenga handaki lake katika eneo la Mar-a-Lago, Maafisa wa Marekani walikuwa wakipanga mikakati ya kumjengea rais Truman katika ikulu ya whitehouse.
Maafisa hao walitaka eneo lililojificha ambapo kutakuwa na afisi zote za serikali.
Eneo la juu la mlima Weather karibu na Bluemont, Virginia ulibadilishwa na kujengwa handaki kubwa la rais , washauri wake na wengine kujificha iwapo kungetokea shambulio.
Wanachama wa bunge la Congress wangepelekwa katika handaki karibu na mgahawa wa White Sulphur Springs, Magharibi mwa Virginia.
Handaki hilo lilikuwa na jina la siri , Project Greek Island, na lilitumiwa kwa miongo kadhaa hadi lilipogunduliwa katika vyombo vya habari 1992 wakati lilipoachwa kutumiwa.
Mlima Weather sasa unasimamiwa na shirika la Federal Emergency Management Agency (Fema) na lilianza kutumiwa tena kufautia shambulio la al-Qaeda la mwezi Septemba 2001.
Handaki la Mlima Weather lilitengezewa rais
Image captionHandaki la Mlima Weather lilitengezewa rais
Handaki hilo liliweza kumlinda Trump wakati wa shambulio,
Watu wanaoishi katika eneo hilo wanataka kujua kuhusu Mlima Weather ama mji wa siku ya mwisho kama unavyojulikana.
Wakati wa majira ya vuli, 1961 ujenzi wa handaki jingine la rais ulianza .
Handaki hilo lilijengewa rais John F Kennedy mjini Florida. Haliko mbali na handaki la Mar-a-Lago - wanamaji wa Marekani walijenga handaki hilo katika kisiwa cha peanut , ikiwa ni umbali wa safari ya dakika kumi kutoka nyumba ya Palm Beach ambapo Kennedy aliishi.
Handaki la Kennedy lilijengwa kumlinda dhidi ya mionzi
Image captionHandaki la Kennedy lilijengwa kumlinda dhidi ya mionzi
Handaki hilo lililojulikana kama hoteli kwa jina Detachment liligharimu $97,000 kulijenga kulingana na repoti ya bunge la Congress 1973 .
Kennedy alizuru eneo hilo mara kadhaa .
Chupa ya maji katika handaki
Image captionHandaki la Kennedy liliwekwa vitu vya kawaida
Mahandaki ya rais , iwe lile la Mlima Weather, katika kisiwa cha Peanut Island ama hata Mar-a-Lago, yalijengwa wakati wa vita baridi.
Blackman anasema kuwa hakuona haja ya kuliimarisha handaki la Mar-a-Lago la rais Trump.
''Iwapo kutakuwa na shambulio la kinyuklia hakuna pa kujificha'' ,anasema Blackman. Handaki hilo lilitumiwa kuwekea meza na viti.
Lakini bado Blackman anasema kuwa anaelewa .Ananiambia kwamba anelewa na iwapo dunia itaangamizwa ataelekea kujificha katika nyumba yake.

Ni akina nani wanaoruhusiwa kuingia katika handaki la rais?

Kisiwa cha Peanut: Rais na washauri wake wachache pamoja na makatibu wake. Kulikuwa na chumba cha watu 30.
Ikulu ya White House: Makamu wa rais Dick Cheney alifanya kazi ndani ya handaki lililo na milango ya chuma wakati wa shambulio la Septemba 11 kulingana na Darling akiwa pamoja na mkewe ; Mshauri wa serikali kuhusu maswala ya usalama Condoleezza Rice, waziri wa ulinzi Donald Rumsfeld, na wengine. (Rais George W Bush alikuwa ndani ya ndege ya Air Force One.)
Mlima Weather: Kuna chumba cha rais , washauri wake na watu wengine hata waandishi ,chumba cha wanahabri killijengwa.

No comments:

Post a Comment