TANGAZO


Sunday, February 11, 2018

Israel yaionya Iran baada ya kufanya mashambulizi Syria

Crash site of an Israeli F-16 jet in northern Israel. Photo: 10 February 2018

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionIsrael inasema kuwa ilishambulia vituo vya Syria na Iran nchini Syia ambapo ndege yake ya F-16 ilishambuliwa na baadaye ikaanguka.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema kuwa nchi yake itajilinda dhidi ya shambulizi lolote baada ya Israel kuendesha mashambulizi yake makubwa zaidi dhidi ya vituo nchini Syria kwa miongo kadhaa.
"Hii ni haki yetu na jukumu letu na tutaendelea kufanya hivyo ikiwa itahitajika," alisema siku ya Jumamosi.
Israel iliendesha mashambulizi dhidi ya vituo vya Iran baada ya kusema kuwa ilikuwa imeikabili ndege isiyo na rubani ya Iran.
Uwepo wa Iran nchini Syria umezua wasi wasi nchini Israel.
Bw Netanyahu alionya kuwa sera za Israel kujilinda dhidi ya lolote na kudhuru watu wake ziko wazi.
"Iran ilikiuka uhuru wa Israel," alisema , akiongeza "ndege isiyo na rubani ya Iran ilitumwa kutoka Syria kuja Israel.
Iran imekana madai ya Israel kuhusu ndege isiyo na rubani.
remains of a missile that crashed earlier in Alonei Abba, east of Haifa, in northern Israel.Haki miliki ya pichaJACK GUEZ
Image captionMabaki ya ndege ya Israel ya F-16
Netanyahu alisema kuwa Israel itapinga jaribio lolote la Iran kuingia kijeshi nchini Syria.
Lakini pia alisema wakati wa mkutano na wakuu wa jeshii kuwa Israel inataka kuwepo amani.

Ni kipi kilisababisha mashambulizi hayo?

Jeshi la Israel linasema kuwa moja ya helikopta zake iliangusha ndege isiyo na rubani iliyoingia nchini mwake siku ya Jumamosi.
Kujibu, Israel inasema kuwa ilishambulia vituo vya Syria na Iran nchini Syia ambapo ndege yake ya F-16 ilishambuliwa na baadaye ikaanguka.
Marubani wawili walifanikiwa kuruka salama kabla ya ndege hiyo ianguke katika eneo lililo karibu na mji wa Harduf kaskazini mwa Israel.
Israel inasema kuwa ilifanya mashambulizi ya pili ya angani dhidi ya vituo vya jeshi vya Syria na Iran.
Jeshi la Israel lilisema kuwa lilifanya uharibifu mkuwa katika vituo hivyo kwenye mashambulizi makubwa zaidi ya aina yake tangu vita vya Lebanon vya mwaka 1982.
Vyombo vya habari nchini Syria vinasema mifumo ya ulinzi ya ilirusha makomboa dhidi ya mashambulizi ya Israel na kugonga zaidi ya ndege moja.
map
Image captionRamani

No comments:

Post a Comment