TANGAZO


Thursday, February 8, 2018

Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini atatembelea K Kusini kwa ajili ya michezo ya Olimpiki

An undated picture released by the North Korean Central News Agency (KCNA) on 12 March 2015 shows North Korean leader Kim Jong-un (C) touring a military unit on an island off the North Korean mainland near the sea border with South Korea in the East Sea.

Haki miliki ya pichaKCNA
Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na mwanamke aliye na ushawishi mkubwa Korea Kaskazini atahudhuria michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi yatakayo zinduliwa Pyeongchang, siku ya Ijumaa, mawaziri jijini Seoul wanasema.
Kim Yo-jong, atakuwa ndugu wa kwanza wa karibu katika familia ya Kim atakayevuka mpaka.
Korea mbili zitaandamana pamoja chini ya bendera mmoja katika sherehe za uzinduzi.
Ushiriki wa Korea Kaskazini umeonekana kama kulegeza uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Hata hivyo, Marekani na Japan wameishtumu Korea Kaskazini kwa kutumia michezo hiyo kama chama cha propaganda.
Kim Yo-jong ni nani?
Akiaminiwa kuzaliwa mwaka 1987, ni mtoto wa kike wa mwisho wa hayati kiongozi Kim Jong-il na ni dada yake wa tumbo moja Kim Jong-un. Anazidiwa umri na kaka yake kwa miaka minne na inasemekana kwamba wana uhusiano wa karibu sana.
Anasemekana kuolewa na mwana wa Choe Ryong-hae, katibu wa chama tawala.
Kim Yo-jong at an opening ceremony of a newly constructed residential complex in Ryomyong street in PyongyangHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKim Yo-jong akiwa kwenye sherehe ya kuzindua jengo la gorofa la makazi Pyongyang 2017
Kim Yo-jong amekuwa akionekana sana miaka ya hivi karibuni, ikiwa kazi yake kuu ni kulinda muonekano wa kaka yake kupita cheo chake kwenye idara ya propaganda ya chama.
north korea family tree
Image captionFamilia yenye usiri zaidi Korea Kaskazini

No comments:

Post a Comment