Hospitali nchini Afrika Kusini ziko kwenye tahadhari kubwa kumpata mwanamume mwenye uume wenye majeraha, baada ya mwanamke mmoja mja mzito kufanikiwa kuuma uume wa mbakaji wake wakati akimdhulumu mbele ya mtoto wake.
Mwanamke huyo alidhulumiwa kingono baada ya kukubali kubebwa kwa gari na wanaume wawili katika mkoa wa Mpumalanga alipokuwa akienda kwa zahanati akiandamana na mtoto wake wa miaka mitano.
Badala yake, gari liliendeshwa kwenda vichakani na akabakwa baada ya kutishiwa kwa kisu, kwa mujibu wa polisi.
Sasa wanaamini kuwa majeraha yake yanaweza kusababisha afikishwe mbele ya sheria.
Polisi wanasema kuwa wanaume hao walikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Tazz karibu na mji wa White River
Kisha wakamtishia mwanamke huyo ambaye ana mimba ya miezi mitatu kwa bunduki na kumuonya asipige nduru.
Baada ya kumuuma, mshambuliaji wake alitoroka na hadi sasa hajapatikana.
Ubakaji na dhuluma za kingano ni tatizo kubwa nchini Afrika Kusini. Visa 109 vya ubakaji viliripotiwa kila siku mwaka 2016/17 na kufikisha idadi hiyo kuwa visa 39,828.

No comments:
Post a Comment