Pages

Wednesday, January 10, 2018

NAIBU WAZIRI DKT. NDUGULILE AITAMBULISHA PROGRAMU YA KIKUNDI MLEZI KWA WANAWAKE WAJASILIAMALI MKOANI KIGOMA

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia mbegu za mise zinazotokana na zao la michikichi zinazotumika kuzalisha mafuta yakutengeneza sabuni katika Kikundi cha Wanawake Wajasiliamali cha Hisani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW)
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akiangalia mashine inayotumika kuchakata mbegu za mise zinazotumika kuzalisha mafuta yakutengenezea sabuni katika Kikundi cha Wanawake Wajasiliamali cha Hisani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki kufanya shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya  sabuni za mise ya michikichi katika Kikundi cha Wanawake cha Nuru Wajasiliamali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.  
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia bidhaa ya mashuka yanayotengenezwa na Kikundi cha Wanawake Wajasiliamali cha Nuru kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitoa motisha ya fedha na kuwaunganisha na moja ya Kikundi cha Wanawake Wajasiliamali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji ambao bado  wachanga na kikundi kilichoendelea kwa ajili ya kulelewa na wajasiliamali waliokuwa katika shughuli za biashara ili wawasaidie kuendeleza biashara zao kupitia Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wanawake kushiriki kuanzisha viwanda vidogo ili kuinua vipato vyao.   
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na Wanawake Wajasiliamali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji katika mwendelezo wa utekelezaji wa  Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ kwa lengo la kuwashirikisha wanawake wajasilimali waliokomaa katika mpango wa kuwasaidia wanawake wajasiliamali wanaoanza shughuli hizo ili kujikwamua kimaisha alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wanawake kuanzisha viwanda na kushiriki shughuli za maendeleo yao. 
Baadhi ya Wanawake Wajasiliamali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile katika mwendelezo wa utekelezaji wa  Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ yenye lengo la kuwashirikisha wanawake wajasilimali waliokomaa katika biashara ili kuwasaidia wanawake wajasiliamali wanaoanza shughuli hizo waweze kujiendeleza pindi alipofanya ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Baadhi ya Wanawake Wajasiliamali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile katika mwendelezo wa utekelezaji wa  Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ yenye lengo la kuwashirikisha wanawake wajasilimali waliokomaa katika biashara ili kuwasaidia wanawake wajasiliamali wanaoanza shughuli hizo waweze kujiendeleza pindi alipofanya ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo. 
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi akifafanua madhumuni ya programu ya ‘kikundi Mlezi’ na malengo yake kwa wanawake wajasiliamali wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile yenye lengo la kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo. 
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe akimshukuru Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kwa jitihada zinazofanywa na maafisa maendeleo ya jamii katika kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) katika ziara ya Naibu Waziri huyo kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo. 
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananwake wajasiliamali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji mara baada ya kumaliza mwendelezo wa utekelezaji wa Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ yenye lengo la kuwashirikisha wanawake wajasilimali waliokomaa katika biasharakuweza kuwasaidia wanawake wajasiliamali wanaoanza shughuli hizo la alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsaha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ameendelea kuitambulisha programu ya ‘Kikundi Mlezi’ yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasilimali kuwa na mfumo wa kuwezeshana  wao wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya biashara.

Dkt. Ndugulile ameitambulisha programu hiyo wakati alipofanya ziara Wilayani Kigoma Ujiji mkoani Kigoma katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kushiriki ipasavyo katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa  ili kufanikisha kufikia Tanzania ya viwanda Serikali itaendelea kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo hasa wanawake katika kuwawezesha kuanzisha vikundi vitakayopanua uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Ameongeza kuwa lengo la kuzindua na kuendeleza  Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ ni kuwashirikisha wanawake wajasilimali waliokomaa katika biashara kuwasaidia wanawake wajasiliamali wanaoanza shughuli za biashara ili kusisimua ukuaji wa uchumi na wa viwanda.

“Niseme programu hii niliyoizindua Wilayani Kiisarawe itaendelea kusaidia kwa asilimia kubwa kuibua wanawake ambao hawakuwa na uwezo katika kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote amesema kuwa programu ya Kikundi Mlezi itasaidia kuwainua wanawake na kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji ili kufikia azma kuwa na viwanda 100 kwa kila mkoa hapa nchini.

“Tutaendelea kushirikiana na Wizara kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi”. Alisisitiza Dkt. Chaote.

Mmoja wa wanawake wajasiliamali Wilayani Kigoma Ujiji Bi. Sophia Ibrahim ameishukuru Serikali kwa kuzindua Mpango huo utakaowawezesha wanawake kusaidiana katika kuanzisha na kuchochea ukuaji wa vipato vyao kutokana na kujenga mfumo wa wanawake kusaidia kujikwamua kiuchumi.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amefanya ziara ya siku mbili mkoani Kigoma na kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake kujishughulisha na miradi ili kusaidia kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.

No comments:

Post a Comment