Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Tido Mhando amefikishwa mahakamani leo jijini Dar es Salaam kwa mashtaka ya matumizi mabaya ya Madaraka.
Tido Mhando, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media alifikishwa katika mahakama ya Kisutu mapema leo Ijumaa, na kusomewa dhidi mashtaka yake.
Anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, wakati alipokuwa akilitumikia shirika hilo la Utangazaji la Serikali TBC, pamoja na kulitia hasara ya shilingi 897 milioni za Tanzania.
Hata hivyo ameachiwa kwa dhamana.
Mkurugenzi wa sasa wa TBC Dkt Ayoub Rioba ameambia BBC kwamba hawezi kuzungumzia taarifa hizo za kufikishwa mahakamani kwa Tido Mhando kwa sasa kwa kuwa "amezisikia pia katika mitandao ya kijamii."


No comments:
Post a Comment