TANGAZO


Wednesday, January 10, 2018

California: Maporomoko ya ardhi yaua watu 13 Marekani

Boulders block a road after a mudslide in Montecito, California.

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBarabara nyingi zimezibwa na mawe makubwa
Watu 13 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kusini mwa jimbo la California, Marekani, maafisa wamesema.
Wengine 163 wamelazwa hospitali, 20 wakiwa na majeraha yanayohusiana na mvua kubwa.
Wanne wana majeraha mabaya.
Watu wapatao 300 wanadaiwa kukwamba katika hori ya Romero, mashariki mwa mji wa Santa Barbara.
Polisi wamesema eneo lililokumbwa na maporomoko hayo linafanana na "uwanja wa vita wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia".
boulders the size of cars slammed into roadwaysHaki miliki ya pichaTWITTER/ @ELIASONMIKE
Image captionMawe makubwa yalimeguka kutoka milimani na kuziba barabara
Mafuriko na maporomoko ya ardhi yameathiri baadhi ya maeneo ambayo yaliathiriwa na moto mkubwa wa nyika na yameharibu barabara kuu ya pwani umbali wa maili 30 (48km).
Maafisa wa uokoaji wamesema kuna watu kadha ambao hawajulikani waliko na kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda.
Maafisa wa Kikosi cha Ulinzi Baharini wametuma ndege kadha kusaidia juhudi za uokoaji na wametahadharisha umma dhidi ya kutumia ndege zisizo na marubani kwani zitatatiza juhudi za uokoaji.
Maelfu ya wakazi wa California waliamrishwa kuondoka makwao Jumatatu, mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili. Mara ya kwanza ilikuwa ni kwa sababu ya moto, wakati huu ni kwa sababu ya mvua.
A search dog looks for victims in damaged homes after a mudslide in Montecito, California.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMbwa wa polisi akiwatafuta manusura eneo la Montecito
bulldozer clearing mud from a road

No comments:

Post a Comment