Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (aliyejishika mdomo), akitafakari jambo, wakati akiwa katika eneo ilipotokea ajali ya kuripuka moto uliosababishwa na kuvuja kwa gesi baada ya bomba lake kupasuliwa na kijiko cha Dawasco, kilichokuwa kikichimba mtaro wa kuweka bomba la maji safi katika Barabara ya Buguruni kwenda Vingunguti jijini Dar es Salaama jana, maeneo ya Buguruni Mnyamani.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mafundiwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), wakifungua nyaya kwenye kipozea umeme (transfoma), baada ya nguzo zake pamoja na nyaya zake kuunguzwa na moto uliosababishwa na kuvuja kwa gesi baada ya bomba lake kupasuliwa na kijiko cha Dawasco, kilichokuwa kikichimba mtaro wa kuweka bomba la maji safi katika barabara ya Buguruni kwenda Vingunguti jijini Dar es Salaama jana maeneo ya Buguruni Mnyamani.
Wananchi wakiangalia sehemu lilipotokea tukio la kupasuka bomba la gesi na kuwaka moto uliosababisha kuungua nyumba, nguzo za umeme pamoja na baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara maeneo ya Buguruni Mnyamani Relini.
Mafundi wa Tanesco, wakiwa kazini wakifungua nyaya kwenye kipozea umeme (transfoma), baada ya nguzo zake pamoja na nyaya zake kuunguzwa na moto uliosababishwa na kuvuja kwa gesi baada ya bomba lake kupasuliwa na kijiko cha Dawasco, maeneo ya Buguruni Mnyamani, jijini Dar es Salaama jana.
Nyumba iliyoungua na kuteketea kabisa kutokana na moto huo wa gesi.
Moja ya nyumba iliyoungua kutokana na moto huo.
Mafundi wa Tanesco, wakiwa kazini wakifungua nyaya kwenye kipozea umeme (transfoma), baada ya nguzo zake kuungua kwa moto huo, maeneo ya Buguruni Mnyamani, jijini Dar es Salaama jana.
Nyumba iliyoungua baadhi ya sehemu yake kutokana na moto huo wa gesi.
Baadhi ya Wahandisi wa Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania, wakiwa katika eneo la tukio hilo
Baadhi ya wananchi wakiwa katika eneo hilo, wengine wakiendelea na shughuli zao za kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kulia), akikabidhi sehemu ya chakula kwa famili iliunguliwa na nyumba pamoja na vifaa vyao, katika eneo la tukio hilo, Buguruni Mnyamani leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kulia), akikabidhi fedha za kujikimu kwa kiongozi wa famili hiyo, Hassan Simba, ambayo nyumba yao iliungua kutokana na moto huo, Buguruni Mnyamani leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kulia), akizungumza na familia hiyo, mara baada ya kabidhi sehemu ya chakula na fedha za kujikimu, Buguruni Mnyamani leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment