Wanasayansi wamepata picha za kwanza za msituni za kati ya nguruwe wachache wenye sura mbaya zaidi duniani.
Nguruwe hao kwa jina Javan waty, wako kwenye hatari ya kuwindwa na kupotea kwa makaazi yao, na wanasayansi wanasema kuwa nguruwe hao tayari wanaelekea kuangamia.
Kamera fiche kwa sasa zimefichua kuwa idadi ndogo wa nguruwe hao bado wanaishi maeneo ya misitu kadha huko Java.
Wanasayansi wanasema kuwa lengo lao ni kulinda makazi ya wanyama hao.
Mkuu wa utafiti huo Dr Johanna Rode-Margono, alisema kuwa wanasayansi walifurahishwa kugundua kuwa nguruwe hao bado wako.
Utafiti wa mwisho kwenye misitu hiyo ulifanywa mwaka 2004 na kuonyesha kuwa idadi ya nguruwe hao ilikuwa ikididimia zaidi.
"Tuliogopa kuwa wote au wengi zaid walikuwa wametoweka," aliiambia BBC.
Kati ya maeneo saba ambayo wanasayansi waliyafanyia uchunguzi wakitumia kamera fiche, ni matatu tu yaligunduliwa kuwa na nguruwe hao.
No comments:
Post a Comment