Rais DonaldTrump wa Marekani, amelipongeza baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini.
Bwana Trump ameandika katika mtandao wake wa Twitter, kwamba hatua hiyo ni ishara wazi kwamba ulimwengu unataka amani na wala sio mauti.
Vikwazo hivyo vilivyowasilishwa na Marekani vinaungwa mkono na China ambaye ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini.
Kufuatia vikwazo hivi vipya uagizaji mafuta wa Pyongyang utapunguzwa hadi asilimia tisini, huku raia wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni wakitakiwa kurudi makwao.
- Trump: Korea Kaskazini wasitujaribu sisi
- Trump: Korea Kaskazini watakuwa kwenye 'shida kubwa'
- Trump aiorodhesha Korea Kaskazini kuwa nchi 'inayofadhili ugaidi'
Wizara ya mambo ya nje ya Uchina imesema vikwazo hivyo havitarajiwi kuwa na athari kubwa za kibinadamu.
Hata hivyo imetowa wito kwa pande zote kushauriana ili kujaribu kupunguza taharuki katika rasi ya Korea.

No comments:
Post a Comment