Papa Francis amewahimiza waumini wa kanisa la Roma Katoliki wasiwatupia mgongo mamilioni ya wahamiaji ambao wamefukuzwa kutoka makaazi yao wakati wa misa kabla ya Krismasi
Kiongozi huyo wa dini aliwafananisha wahamiaji na Maria na Yosefu kutoka Bibilia, na namna ambavyo walivyosafiri kutoka Nazareti hadi Bethlehemu bila kupata makazi.
Alieeleza kuwa wahamiaji wengi wanalazimika kukimbia viongozi wao ambao 'hawaoni tatizo na kumwaga damu ya wasio na hatia"
Papa Francis amefanya uteteaji wa wahamiaji kama maadhui yake kuu katika uongozi wake.
Idadi ya wakimbizi duniani imezidi milioni 22, ikiwa idadi kubwa ikitokea kwa warohingya kukimbia uhalifu nchini Myanmar.
"Nyayo zao zimefichwa kwenye nyayo za Yosefu na Maria,' alielezea Papa Francis, ambaye yeye pia ni mjukuu wa wahamiaji kutoka Italia, kwa washirika wa kanisa la St Peters mjini Vatican, jioni ya Jumapili.
Kiongozi huyo wa waumini waroma katoliki takriban bilioni 1.2 amesisitiza kuwa imani yao inataka wageni wakaribishwe kila mahali.
Papa Francis anatarajiwa kutoa hotuba yake ya "Urbi et Orbi", yaani "kwa mji na kwa dunia" siku ya Jumatatu.
No comments:
Post a Comment