Mwenyekiti wa Baraza la Watoto wa Wilaya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Yusra Mohamed kulia pamoja na Katibu wa Baraza la Watoto Mkoa wa Arusha Raphael Denis kushoto mara baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa kuiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa kimataifa wa kuzuia ukatili dhidi ya watoto utakaofanyika Nchini Swedeni Februari 2018.
MWENYEKITI wa Baraza la Watoto wa Wilaya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Yusra Mohamed pamoja na Katibu wa Baraza la Watoto Mkoa wa Arusha Raphael Denis wamechaguliwa na wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa kuiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa kimataifa wa kuzuia ukatili dhidi ya watoto utakaofanyika Nchini Swedeni Februari 2018.
Watotao hao wamechaguliwa baada ya kupita katika Mchujo mkali uliowakutanisha wagombea kutoka Mikoa ya Bara na Visiwani na wataiwakilisha Tanzania katika Mkutano huo ambao Tanzania ni moja ya Nchi chache Barani Afrika kupewa kipaumbele cha ushiriki kufuatia hatua kubwa iliyofikia katika juhudi zake za kupambana na ukatili dhidi ya watoto.
Kwasasa Tanzania inatekeleza mkakati wake wa miaka mitano wa kutokomeza kabisa ukatili dhidi ya wanawaka na watoto unaotekelezwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau mbalimbali wa wanaopambanakuhakikisha Tanzania inakomesha kabisa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment