Mufti Sheikh Abubakari Zubeir bin Ally akimkabidhi tuzo ya shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa hafla fupi ya kumaliza kambi ya siku nne ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab iliyofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia. Kushoto ni Balozi wa Saudi Arabia Nchini Mhe. Mohamed bin Mansour Al Malik.(Picha zote na JKCI).
Balozi wa Saudi Arabia Nchini Mhe. Mohamed bin Mansour Al Malik akimkabidhi tuzo ya shukrani Mufti Sheikh Abubakari Zubeir bin Ally katika hafla fupi ya kumaliza kambi ya siku nne ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab iliyofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia. Jumla ya wagonjwa 33 walifanyiwa upasuaji katika kambi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akiishukuru Serikali ya Saudi Arabia kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchi hiyo kwa kutuma wataalamu wake hapa nchini kutoa huduma ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Jumla ya wagonjwa 33 walifanyiwa upasuaji katika kambi hiyo.
Madaktari bigwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saud Arabia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufanya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa wagonjwa 33.
Jengo la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete

MADAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saudi Arabia wamefanya upasuaji wakuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa wagonjwa 33.
Kwa mara ya kwanza tangu Taasisi imeanza kutoa huduma ya matibabu ya upasuaji wa Moyo bila ya kufungua kifua tumefanya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono. Upasuaji tuliokuwa tunaufanya kwa wagonjwa wetu ni wa kutumia mishipa ya paja.
Upasuaji wa moyo unaofanyika katika kambi hii ambayo imeanza Jumatano tarehe 15/11/2017 hadi Jumamosi tarehe 18/11/2017 ni ya upasuaji wa bila kufungua kifua kwa watu wazima. Upasuaji uliofanyika ni wa kuzibua mishipa ya moyo iliyoziba.
Faida ya upasuaji uliofanyika ni kumwezesha mgonjwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa anatembea na baada ya masaa manne kama hali yake inaendelea vizuri anaweza kuruhusiwa. Tofauti na upasuaji wa kutumia mshipa wa paja ambao tulikuwa tunaufanya, baada ya upasuaji mgonjwa ni lazima akae Hospitali kwa zaidi ya masaa 24 ili kuangalia maendeleo ya afya yake.
Kambi hii imeenda sambamba na utoaji wa elimu na kubadilishana ujuzi wa kazi kati ya wafanyakazi wa Taasisi hizi mbili ikiwemo aina mpya ya upasuaji uliofanyika kitu ambacho kimewajengea uwezo zaidi wafanyakazi wetu. Aidha wageni nao wamepata muda wa kujifunza vitu vingi na kupata uzoefu mpya wa baadhi ya magonjwa na mambo ya kiteknolojia ambayo katika nchi yao hakuna.
Tunaendelea kuwasisitiza wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na hivyo kupata tiba kwa wakati. Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika matibabu ya wagonjwa wetu ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri.
Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapougua na kuhitaji kupata matibabu.
Kwa namna ya kipekee tunaishukuru sana Taasisi ya Kimataifa ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) kwa kutuma wataalam wake wa magonjwa ya moyo kuja hapa nchini kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa wetu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
18/11/2017

No comments:
Post a Comment