TANGAZO


Friday, October 6, 2017

Syria waweka hai matumaini ya Kombe la Dunia

Omar Al Somah

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMshambuliaji wa Syria Omar Al Somah huchezea Al Ahli ya Saudi Arabia
Omar Al Somah alifunga bao kupitia mkwaju wa penalti dakika za mwisho na kuweka hai matumaini ya Syria kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 kwa kutoka sare ya 1-1 na Australia.
Katika mechi yao ya awali, mshambuliaji Al Somah alifunga bao dakika za mwisho dhidi ya Iran na kulazimisha sare na iliyowawezesha kumaliza wa tatu katika kundi lao la kufuzu kwa Kombe la Dunia katika bara Asia.
Alifunga bao hilo la kusawazisha Alhamisi nchini Malaysia - ambapo Syria huchezea mechi zao za nyumbani - baada ya kuwa nyuma kutokana na bao la Robbie Kruse.
Mechi ya marudiano itachezwa Sydney Jumanne ijayo.
Mshindi atakutana na timu nyingine kutoka shirikisho la Concacaf kwenye mechi mbili (ya nyumbani na ya ugenini) kuamua timu itakayofuzu kwa Kombe la Dunia.
Syria players celebrateHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSyria walisherehekea sana, mashabiki na wachezaji, baada ya bao hilo la kusawazisha

No comments:

Post a Comment