KAMPUNI ya Ulinzi ya SGA imezindua chata mpya ya huduma kwa wateja ikiwa ni sehemu ya maadhinisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Akizindua chata hiyo mpya, Mkurugenzi Mtendagi wa SGA Tanzania, Eric Sambu alisema kampuni hiyo inaweka mikakati madhubuti ili kuendana na matakwa na mahitaji ya wateja wao hasa katika mazingira ya sasa ya biashara ambayo yanabadilika kila kukicha.
Alisema kuna mabadiliko mengi mno katika soko na hivi kulazimu makampunni mengi kufanya mabadiliko ili kuendanana na hali halisi na makampuni mengi bado hayajaweza kusimama imara.
“Ili kuendana na hali halisi ya sasa hivi ni lazima tuendane na mazingira yalivyo ili tuweze kutoa huduma nzuri kwa wateja wetu,” alisema Bw. Sambu.
Alisema SGA inaadimisha miaka 33 nchini Tanzania huku ikiwa imepata mafanikio mazuri hasa katika miaka mitano iliyopita na kusisitiza kuwa wameweza kupata mafanikio haya kutokana na kuboresha utendaji kazi, kuwezesha wafanyakazi kupitia mafunzo mbalimbali katika vitengo vyote. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, chata hii mpya inamlenga mteja zaidi katika utendaji wa SGA.
“Mabadiliko ya hivi karibuni katika ufanyaji biashara Tanzania yametupa fundisho kubwa na nafasi ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wetu wote katika ngazi zote ili waweze kuwahudumia wateja vizuri zaidi na kukidhi matakwa mapya ya soko sasa hivi na hili kwetu sasa hivi limekuwa jambo la kawaida,”
“Tunaendelea kuboresha mifumo yetu na kuwekeza zaidi katika teknolojia na rasilimali watu ili kuhakikisha tunafanya vizuri. Tumeweza kuhakikisha tunapata hati safi katika usimamizi wa ubora tangu mwaka 2001 (ISO certification on Quality Management System) na hivi karibuni tumepata hati safi ya afya na usalama (Occupational Health and Safety ISO 18001 Standard).
Meneja wa Uhusiano wa Wateja wa SGA, Aikande Makere, alisema wanaamini chata hii mpya itahakikisha kuwa wateja na wadau wote wanapokea huduma wanayostahili kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia uaminifu, uwajibikaji, usawa na wepesi wa kubadilika kulingana na mazingira.
“Tunawashukuru wateja wetu wote ambao wamekuwa pamoja nasi hata katika kipindi hiki chenye changamoto kubwa katika biashara,” alisema Aikande.
SGA ndio kampuni kongwe ya binafsi ya ulinzi nchini Tanzania huku ikiwa imeajiri zaidi ya watanzania 5100 katika maeneo ambayo wanafanya biashara Tanzania. Wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo ulinzi kwa kutumia maaskari, ulinzi kwa kutumia umeme, huduma za dharura (emergency response), ufuatiliaji (tracking), usafirishaji wa mizigo na vifurushi (courier) na usafirishaji wa fedha.
“Tuna magari 222 na vituo 12 nchi nzima ambavyo vina mitambo ya kisasa na wafanyakazi waliobobea katika masuala ya ulinzi na tumehakikisha kuwa tuna miundombinu madhubuti ya kuwahudumia wateja wetu nchi nzima.,” alisema Sambu.
No comments:
Post a Comment