TANGAZO

Tuesday, October 17, 2017

HALOTEL YAJIVUNIA MAFANIKIO MIAKA 2 YA KUTOA HUDUMA TANZANIA

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari, (hawapo pichani) wakati kampuni hiyo, ilipokuwa ikitoa taarifa ya utendaji kwa miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. Kampuni hiyo, imejivunia mafanikio iliyoyapata kutokana na mazingira bora ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali pamoja na kutoa ajira za moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 1200 na kuwa na wateja zaidi ya milioni tatu na laki tano (3.5). Pamoja nae katika picha ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Trieu Tanh Binh. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari, (hawapo pichani) wakati kampuni hiyo, ilipokuwa ikitoa taarifa ya utendaji kwa miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. Kampuni hiyo, imejivunia mafanikio iliyoyapata kutokana na mazingira bora ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali pamoja na kutoa ajira za moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 1200 na kuwa na wateja zaidi ya milioni tatu na laki tano (3.5). Pamoja nae katika picha katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Trieu Tanh Binh na kushoto ni Meneja Mawasiliano, Hindu Kanyamala. 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari, (hawapo pichani) wakati kampuni hiyo, ilipokuwa ikitoa taarifa ya utendaji kwa miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. Kampuni hiyo, imejivunia mafanikio iliyoyapata kutokana na mazingira bora ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali pamoja na kutoa ajira za moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 1200 na kuwa na wateja zaidi ya milioni tatu na laki tano (3.5). Pamoja nae katika picha katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Trieu Tanh Binh na kushoto ni Meneja Mawasiliano, Hindu Kanyamala. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari, (hawapo pichani) wakati kampuni hiyo, ilipokuwa ikitoa taarifa ya utendaji kwa miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. Kampuni hiyo, imejivunia mafanikio iliyoyapata kutokana na mazingira bora ya uwekezaji yaliyowekwa na Serikali pamoja na kutoa ajira za moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 1200 na kuwa na wateja zaidi ya milioni tatu na laki tano (3.5). Pamoja nae katika picha katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Trieu Tanh Binh na kushoto ni Meneja Mawasiliano, Hindu Kanyamala. 

Dar es Salaam, 17 Octoba 2017 .
IKIWA inaadhimisha Miaka miwili tangu kuanza utoaji wa huduma za mawasiliano nchini Tanzania, Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Halotel imetangaza kupata mafanikio Makubwa katika sekta ya Mawasiliano huku ikijivunia mapinduzi makubwa ambayo imeleta katika sekta hiyo tangu kuanza kutoa huduma zake nchini.

Akizungumzia mafanikio hayo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Bwana. Trieu Than Binh, amesema kuwa katika miaka miwili ya utoaji huduma, wamefanya mapinduzi na mabadiliko makubwa katika sekta hiyo katika nyanja za Mawasiliano ikiwemo kuboresha miundombinu ya Mawasiliano, Mabadiliko katika Elimu, huduma za kifedha pamoja na kupunguza gharama za mawasiliano.

“Tangu tumeanza kutoa huduma kwa mwaka wa pili sasa idadi ya wateja imeendelea kuongezeka kwa kasi. Hii inatokana na huduma ambazo tumekuwa tukizibuni kwa pamoja na kuwekeza zaidi katika kutoa huduma bora na kuboresha miundombinu ya mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini.” Alisema Binh na Kuongeza, “Idadi ya wateja wetu imeendelea kukua siku hadi siku na hadi sasa tuna zaidi ya wateja milioni tatu na laki tano (3.5) na bado kila wakati TCRA wanapotoa taarifa za Mawasiliano kampuni yetu imeendelea kuwa kampuni inayoongeza idadi ya wateja. Tunaamini kwa ongezeko tunaloenda nalo hadi kufikia mwisho wa mwaka huu tutakuwa miongoni mwa kampuni tatu bora zenye idadi kubwa ya Wateja.” Alisema.

“Kwanza tunafurahishwa na Serikali kutokana na mazingira bora ya uwekezaji ambayo imeweka hadi sasa,  na pia mazingira mazuri ya ukusanyaji wa kodi kwa uwazi zaidi suala ambalo hata kwetu limeondoa usumbufu kwa kiasi kikubwa, kuzinduliwa kwa kituo cha ukusanyaji kodi kwa njia ya kielectroniki ilikuwa faraja kubwa kwetu na ndio maana tulikuwa miongoni mwa kampuni za kwanza za simu kujiunga na mfumo huo.”

Akizungumzia uhusiano kati ya kampuni yake na Serikali, Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa wanafurahishwa na ushirikiano wanaoupata kutoka katika taasisi mbalimbali za serikali ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa taasisi hiyo, “Tunaishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa Pamoja na Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Mamlaka ya Mapato (TRA) Vyombo vya Usalama kwa pamoja na taasisi nyingine za Serikali ambazo kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakitupatia Miongozo ambayo imechangia ukuaji wetu.” Alisema

Pamoja na mambo mengine Bwana Binh, alisema kuwa wamefurahi pia kuwa kampuni inayoongoza kwa kutoa ajira kwa Maelfu ya Watanzania ikiwa ni ajira za moja kwa moja zaidi ya elfu moja na mia mbili 1200, na ajira zisizo za moja kwa moija zaidi ya Elfu Ishirini 20000 na kusema kuwa kutokana na uwekezaji ambao kampuni hiyo imeendelea kufanya wanaamini wataendelea kuongeza idadi ya ajira nchini.

Aidha Binh, aliongeza kuwa wanaamini bado wana nafasi kubwa zaidi ya kufanya uwekezaji na kubadili kabisa mfumo wa Mawasiliano nchini kwa kuanzisha njia mpya za mawasiliano kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi na kuwa kampuni itakayo ongoza katika utoaji wa huduma za Mawasiliano kupitia Tehama na Teknolojia ya Mawasiliano.

“Kwa sasa tunaelekea kuanzisha mtandao wa 4G LTE kwa wateja wetu wote wa Halotel, hatuta bagua maeneo tutafanya uwekezaji huu katika maeneo yote nchi nzima ili wateja wetu waweze kufurahia huduma bora za mawasiliano na kwa bei rahisi,” alisema na kuongeza, “Pia tunaangazia sekta ya elimu ambayo hadi sasa kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar Es Salaam, tumeweza kuanzisha mfumo wa kujisomea kwa shule za sekondari nchini kwa masomo ya Sayansi Mfumo ambao utapatikana bure kwa shule zote zinazotumia Mtandao wa Intaneti wa Halotel, Tumeanza na masomo ya sayansi na kadri muda unavyokwenda tutaangalia namna ya kuingiza masomo mengine, baada ya kukamilisha kutia saini Mkataba wa Maelewano kati yetu na Wizara ya Utawala bora TAMISEMI.

Alisema Mkurugenzi huyo na kuongeza “Pamoja na kujikita katika kuleta mapinduzi ya Elimu bado pia tunaangazia kuboresha hali ya usalama wa barabarani pamoja na familia, ambapo tunazo teknolojia mfano “Smart Home” hii ni teknolojia inayomuwezesha mzazi kuweza kuangalia mwenendo mzima wa nyumba yake na familia popote atakapo kuwa, au hata mtoto wake anapokuwa au anapotoka nyumbani kwa kumvalisha kifaa maalum,”

Bwana Binh, ameeleza kuwa pamoja na mafanikio hayo, kampuni yake imekuwa ikijitolea katika kurudisha kile wanachokipata kwa jamii ya Watanzania kwa kuendesha Miradi mbalimbali ya kuisaidi jamii, ikiwemo mradi wa kusaidia watoto wenye Matatizo ya vichwa vikubwa na Mgongo wazi, Mradi wa kutoa vifaa vya ujenzi kwa mashule mbalimbali nchini pamoja na mradi wa kusaidia vituo vya watoto yatima na wale wenye uhitaji.

Akihitimisha Mkurugenzi huyo alibainisha baadhi ya Changamoto zinazowakabili alitaja kwa uchache kuwa, ni gharama kubwa ya uendeshaji wa minara ya Mawasiliano katika maeneo ambayo hayana umeme wa uhakika, hivyo kutumia gharama kubwa kuendesha minara hiyo, pamoja na wizi ambao unatokea katika maeneo ya minara hiyo, na kusema kuwa wanaamini changamoto hizo zina muda wake na wanaamini zitakwisha.

Tunawashukuru sana Watanzania ambao ndio wateja wetu, kwani wamekuwa wakituunga sana mkono katika utoaji wa huduma za Mawasiliano, wao ndio walaji wa bidhaa zetu  na tuna waahidi kuwa tutaendelea kusimamia weledi katika kutoa huduma zenye ubora na zitakazo kidhi mahitaji yao, katika kuadhimisha miaka hii miwili tumewaandalia ofa maalumu kila mteja atakae jiunga na kifurushi chochote cha kuanzia Shilingi 500, ataweza kujishindia zawadi ya muda wa maongezi, simu na zawadi nyinginezo na pia pale watakapokuwa wanatembelea maduka yetu na kununua bidhaa mbalimbali wataweza kujishindia zawadi mbalimbali kama simu na muda wa Maongezi.

No comments:

Post a Comment