Inawawezesha wanawake na wanaume kuelewa na kushiriki katika kujenga na kushirikiana ujuzi wanaohitaji ili watoe mchango kikamilifu katika jamii yao. Raia wenye taarifa sahihi huifanya serikali iwajibike. Ufikivu Habari ni dereva wa uvumbuzi na ubunifu, kuongeza fursa kwa wote, hasa kwa wasichana na wanawake. Ufikivu habari huanza na kujitolea kwa Serikali kutengeneza, kueneza na kutekeleza sera na sheria zinazohusu haki ya habari na kuhakikisha kuheshimiwa kwa haki hii ya kibinadamu.
Hii inahitaji utaratibu wa ufanisi wa utekelezaji na utamaduni wa uwazi katika aina zote za taasisi. Wananchi wanahitaji pia kuwa na fikra pana, ujuzi wa kusoma na ujuzi wa kidigitali ambao unahitajika kufikia, kuchambua na kutumia habari kwa njia tofauti, nje na ndani ya mitandao.
Hii ndiyo maana UNESCO inaziomba serikali zote na washirika kutumia uwezo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kusaidia kufikia Lengo la 4, Elimu Endelevu inayolenga kuhakikisha " elimu shirikishi, sawa na ya ubora na kukuza fursa za elimu isiyo na mwisho kwa wote; Ufikivu wa Habari pia unajumuisha kukuza uandaaji wa maudhui yanayofaa, yenye kulenga jamii husika na yanayopatikana kwa lugha mbalimbali. Yote hii inahitaji sera zenye ufanisi na ushirikiano mzuri katika ngazi zote.
Haiwezekani kuwepo kwa ufikivu wa habari kwa wote bila kuwepo kwa vyombo vya habari vilivyo huru. Ufikivu wa habari sio tu ni lengo peke yake; pia ni mchangiaji muhimu katika utekelezaji wa malengo mengine yote ya Maendeleo Endelevu. Kwa hiyo ni muhimu tuendeleze juhudi zetu ili kuhakikisha kuwa kila mwanamke na mwanamume wanafurahia ufikivu kamili wa habari.
No comments:
Post a Comment