Mshambuliaji wa PSG Neymar, 25, ameitaka timu yake mpya kumuuzilia mbali mshambuliaji mwenza Edinson Cavani 30, baada ya kukosana uwanjani siku ya Jumamosi. (Sport via Daily Mail)
Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus anatarajiwa kuandikisha kandarasi mpya na kilabu hiyo akitarajiwa kupata nyongeza maradufu ya kipato cha £150,000 kwa wiki ambazo amekuwa akipata.(Daily Mirror)
Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28. Mchezaji huyo wa Chile pia anasakwa na manchester City. (Sun)
Barcelona ilishindwa kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezman kwa kitita cha £124m, 26, msimu uliopita. Manchester United pia walikuwa wakiisaka saini ya mchezaji huyo wa Ufaransa. (Mundo Deportivo via Talksport)
Tottenham wanapanga kumsajili mshambuliaji wa besikitas Cenk Tosun wakati wa kufunguliwa kwa dirisha la uhamiaji mwezi januari ambaye alizifutia klabu za Crystal Palace na Newcastle msimu uliopita. (Talksport)
Manchester United wanamtaka mshambuliaji wa Genoa Pietro Pellegri, ambaye alifunga mara mbili dhidi ya lazio siku ya Jumapili. (Gazzetta dello Sport via Metro)
Manchester United na Manchester City ni miongoni mwa klabu ambazo zinapanga kumsajili mshambuliaji wa Lazio Sergej Milininkovic-Savic, 22 (Daily Mirror)
Mshambuliaji wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anataka uhamisho wa kuelekea West Ham mnamo mwezi januari kwa kuwa Arsenal haijaanza mazungumzo yoyote ya kumpatia kandarasi mpya(Daily Star)
Real Madrid wanataka kumuuza mshambuliaji Karim Benzema, 29, kwa Arsenal. (Don Balon via Daily Star)
Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mathieu Flamini anaamini bado anaweza kunedelea kucheza.Flamini mwenye umri wa miaka 33 amekuwa ajenti huru tangu alipoondoka Crystal palace mwishoni mwa msimu uliopita. (sun)
Chelsea inachunguzwana Fifaf kwa kukiuka sheria zinazowalinda wachezaji wenye umri mdogo.Klabu hiyo inasema inakubaliana na sheria zaote za Fifa wakati inapowateua wachezaji wake (Daily Mail)
Manchester City wamekuwa wakitumia ushawishi wa kiungo wa kati wa brazil ili kusaidia kupata wachezaji wanaowataka.(Manchester Evening News)
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amewatambua Michael Carrick na Paul Scholes kama wachezaji wawili waliokuwa na athari kubwa katika mchezo wake katika uwanja wa Old Trafford (Daily Mirror)
Wayne Rooney bado atapewa fursa ya kuwa balozi wa Manchester United licha ya kukiri kunywa na kuendesha gari (Daily Star)
Wachezaji wa Barcelona walionyesha kumuunga mkono Ousmane Dembele, ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti kwa kuvaa shati iliokuwa na ujumbe Courage Ousmane kabla ya mechi yao dhidi ya Eiber(Daily Mirror)


No comments:
Post a Comment