Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema hali ya watu wa Rohingya Myanmar ni janga, na kuwataka wenye dhamana ya uongozi nchini Burma kusitisha vurugu katika jimbo la Rakhine .
Antonio Guterres alielezea hali ya makaazi hayo kuwa kama sehemu ya tatu ya utakaso wa kikabila kwa Rohingyas , na kuonya kuwa mgogoro huo unazidi kukua na kugeuka kuwa uharibifu wa kikanda .
Inaarifiwa kuwa mamia ya maelfu ya Waislamu wa eneo hilo la Rohingyas wamekimbilia Bangladesh , na bwana Guterres amesema hali yao ya kibinadamu ni mbaya.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limeshutumu vikali vurugu zinazoendelea katika jimbo la Rakhine , na kusema kuwa hatua za makusudi hazina budi kuchukuliwa haraka iwezekanavyo kusitisha hali hiyo.

No comments:
Post a Comment