Pages

Thursday, September 21, 2017

Je Kenya inaelekea katika mzozo wa kikatiba?

Mahakama ya juu ilitoa uamuzi wa kihistoria kwa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi

Image captionMahakama ya juu ilitoa uamuzi wa kihistoria kwa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi
Kwa kuilaumu tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake kwa kushindwa kuandaa uchaguzi ulio huru na haki, mahakama ya juu imeliweka taifa hilo katika hali ambayo inaweza kusababisha mkwamo wa kikatiba.
Uamuzi wa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi ukiwa ni wa kwanza kufanyika barani Afrika ulipongezwa na waangalizi wengi wa uchaguzi wakisema kuwa ni hatua ya kidemokrasia na utenganishaji wa mamlaka na idara ya mahakama ilio huru.
Lakini pia unatoa swali la iwapo marudio ya uchaguzi yanaweza kufanywa katika muda uliotolewa na katiba.
Uamuzi wa mahakama kwamba uchaguzi huo umefutiliwa mbali ulisomwa kwa urefu siku ya Jumatano, ukiitaja tume ya uchaguzi ilioshindwa kusimamia uchaguzi kwa njia ya kisheria.
Huku uchaguzi mwengine ukitarajiwa mwishoni mwa mwezi Oktoba, hatua hiyo inafungua swali jingine la ni vipi IEBC inaweza kuaminiwa kuandaa uchaguzi mwengine katika wakati unaofaa.
Kampuni iliotoa mfumo wa kielektroniki kwa uchaguzi huo wa kwanza inasema kuwa wakati ni mchache mno kuandaa kila kitu kabla ya Oktoba 31.
Na hiyo ni iwapo pande zote mbili zitakubaliana kuhusu utumizi wa vifaa hivyo vya kampuni ya OT-Morpho kwa uchaguzi wa pili, badala ya kutangaza zabuni nyengine.
Wafuasi wa rais Uhuru Kenyatta wakiandamana na kupinga uamuzi huo wa mahakama ya juu
Image captionWafuasi wa rais Uhuru Kenyatta wakiandamana na kupinga uamuzi huo wa mahakama ya juu
Hawana kandarasi ya kuwasilisha vifaa vyengine.
Upinzani tayari unasema kuwa utasusia marudio hayo ya uchaguzi hadi pale kutakapokuwa na mabadiliko ya maafisa katika tume ya uchaguzi.
Wito wa jaji mkuu wa kuitaka IEBC kuandaa uchaguzi mwengine utasababisha kuchelewa kwa uchaguzi huo bila shaka.
Kabla ya uamuzi huo kusomwa ,rais Uhuru Kenyatta ameapa kwamba uchaguzi huo utafanyika kama ulivyopangwa huku IEBC ikisimamia na katika wakati uliopo.
Lakini uamuzi huo unatilia shaka hatua hiyo.
Tatizo hilo la mkwamo wa kikatiba hatahivyo linaendelea kuzua maswali mengi zaidi ya majibu kuhusu ni nini kitakachofanyika iwapo shughuli hiyo haitafanyika kufikia Oktoba 26.
Je Serikali ya mpito ndio itakayokuwa daraja la muda wa kikatiba uliokwisha na ule ambao uchaguzi mpya utafanyika?
Ni swala ambalo halijafanyika kwa taifa kama Kenya na iwapo viongozi wake watapunguza matamshi ya chuki na uchochezi, hali ya wasiwasi huenda ikapanda.
Jaji mkuu tayari amekosoa ongezeko la vitisho na ushambulizi dhidi ya majaji katika mitandao ya kijamii na zaidi.
Ni wazi kwamba mengi yanafaa kubadilika kabla ya marudio ya uchaguzi kufanyika.
Rais Uhuru Kenyatta anataka tume ya uchaguzi kuandaa uchaguzi mpya bila mabadiliko yoyoteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais Uhuru Kenyatta anataka tume ya uchaguzi kuandaa uchaguzi mpya bila mabadiliko yoyote
IEBC haikufanya uwazi na wala kuhakiki na pia ilikaidi amri ya mahakama kukubali uchunguzi wa sava zake za kompyuta kulingana na uamuzi wa mahakam ya juu.
Kushindwa kwa tume hiyo kuajiri wataalam kukagua mfumo huo uliishinikiza mahakama ya juu kufanya uamuzi usio wa kawaida.
''Hatua hiyo inatuwacha na chaguo moja la kukubali madai ya mlalamishi kwamba mfumo wa kiteknolojia wa IEBC ulidukuliwa'' , alisema naibu jaji mkuu Philomena Mwilu.
''Kwa kukataa kukubali waangalizi waingie katika sava za IEBC ili wajionee iwapo udukuzi ulifanyika au la ni thibitisho tosha kwamba udukuzi huo ulifanyika''.
Mwenyekiti wa tume ya IEBC alikosolewa moja kwa moja kwa kumtanagza rais Uhuru Kenyatta mshindi wa uchaguzi wa urais kabla ya matokeo yote kuhakikiwa.
Upinzani una hoji kwamba hawezi kuendelea na majukumu yake lakini mkakati wa kutaka kumuondoa utachukua muda mrefu na mgumu.
Raila Odinga anahisi alifanyiwa udanganyifu na IEBC na huenda akatumia hatua hiyo kuleta mabadiliko katika tume ya uchaguziHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRaila Odinga anahisi alifanyiwa udanganyifu na IEBC na huenda akatumia hatua hiyo kuleta mabadiliko katika tume ya uchaguzi
Malezo yaliotolewa na mahakama ya juu katika uamuzi wake unathibitisha kwamba uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu mkubwa iwapo sio katika upigaji kura hususan vile matangazo hayo yalivyotolewa, kutangazwa na kuhakikiwa.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ana sababu nyingi za kususia uchaguzi mpya hadi pale mfumo mpya wa kutangaza matokeo utakapobadilika, lakini haujibu swala muhimu la ni nini kitakachotokea baadaye?

No comments:

Post a Comment