Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Dkt Juliana Pallangyo kushoto akipata maelezo ya mradi huo mara baada ya kutembelea kwenye eneo la mtambo huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Mhandisi, Robert Gabriel.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na
Madini, Dkt Juliana Pallangyo
akishiriki kucheza ngoma ya wananchi wa Kijiji hicho mara baada ya
kuzinduaa mradi huo.
|
NI ukweli usiopingika
utekelezaji wa sekta ya viwanda inahitaji nishati ya umeme katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo za uzalishaji
mali ili kuweza kupata mafaniko yanayoweza kusaidia kuinua uchumi
wao.
Kwani bila kuwepo kwa nishati hiyo kwa baadhi ya maeneo hasa
vijijini
kuna pelekea kushindwa kufikia malengo
yao kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa kuhofia iwapo
zitakaa muda mrefu zitaharibika.
Licha ya hivyo lakini pia kukosekana kwa nishati hiyo kuna
sababisha
watanzania wenye nia ya kuanzisha
viwanda vidogo vidogo kukwama kufikia malengo yao waliojiwekea kwa
kuvianzisha.
Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la
Mfuko wa Mitaji na Maendeleo (The United
Nations Capital Development Fund –UNCDF) kwa kushirikiana na kampuni ya
Ensol Tanzania Limited waliamua kuanzisha mradi wa umeme wa jua (sola)
kwenye kijiji cha Mpale Kata ya Mpale wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
Mradi huo ambao umekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kijiji
hicho
umefadhiliwa na Shirika hilo ambao
umelenga kuwasaidia kuondokana na changamoto ambazo zilikuwa
zikiwakabili ikiwemo kutumia vibatari wakati wakienda kujifungua kwenye
zahanati ya Kata hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Diwani wa Kata ya Mpale
Tarafa ya Bungu wilayani Korogwe Mkoani
Tanga,Shemakao Miraji anasema mradi huo ni faraja kubwa kwa wakazi wa
Kijiji hicho na maeneo jirani ikiwemo kufungua fursa za kiuchumi lakini
kuendana sanjari na kauli
mbiu ya serikali ya viwanda.
Anasema awali walikuwa wakilabiliwa na changamoto kubwa ya wakina
mama
wajawazito kwenda kujifungulia kwenye
zahanati hiyo kwa kutumia vibatari jambo ambalo lilikuwa ni hatari kwa
maisha.
Diwani huyo anasema faida kubwa za mradi huo utasaidia kuboresha
huduma za afya kwa wakina mama ambao
walikuwa wakienda kwenye vituo vya afya kwa kutumia vibatari lakini
baada ya kufika umeme huo utawasaidia kuondokana na kadhia hiyo ambayo
ilikuwa ni hatari kwa maisha yao ambao ni nguvu kazi kuelekea uchumi wa
viwanda.
"Kilio kikubwa cha wananchi wetu hapa ni maembe yanayoanguka na
kuoza
ha hatuwezi kupata namna nyengine ya
kuweza kutuepusha na adha ya kuondokana nayo na hii itatusaidia
kuondokana na dhamana hiyo lakini pia umeme huu utatusaidia kuingia kwen
ye uchumi wa kati kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya chai na kukuza zao hilo." Anasema.
Naye kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Dkt Juliana Pallangyo
anawapongeza kampuni hiyo na washirika wa kiufundi TTA kwa juhudi
walizofanya kuchagua kijiji hicho kufanya utafiti, kubuni mradi huo kwa
kutafuta fedha na kutafuta taratibu zote katika
kutekeleza mradi huo huku akiwataka wananchi kuanzisha viwada
vidogo vidogo.
“Katika kutafuta fedha nafahamu Ensol ilifanikiwa baada ya
kushindwa
nishwa na makampuni mengine kwani
taasisi hizi zilizotajwa zinatoa fedha kwa mtindo wa ushindani na
wanapokea maombi mengi ya ufadhili kutoka maeneo mbalimbali ya dunia na
Afrika “Anasema
“Lakini pia nimefurahishwa na zaidi na huduma kadhaa zilizotolewa
na
mradi kwa jamii hii hapa kwanza
kuwawezesha wananchi kuunganishwa na umeme ikiwemo kufanyiwa wayaringi
kwa mkopo “Anasema.
Anasema ni kweli katika maeneo ya vijijini huduma ya umeme imefika
lakini wananchi wengi
wanashindwa kuunganishwa na umeme kwa sababu gharama ya kutandaza
nyaya kwenye nyumba zao.
“Tunawashukuru sana Ensol kwa kufikiria kutatua changamoto hii na
pia
tunawashukuru Power Africa kwa kuunga
mkono jambo hili kwa kutoa fedha na naamini wananchi wa hapa mpale
watatumia fursa ya umeme ambayo sio rahisi kupatikana kuunganishwa nayo
“Anasema.
“Lakini pia ni kwamba nishati hii ya umeme itapatikana kwa saa 24
kwa
siku 7 za wiki bila kukatika hii ni
habari njema kwa watumiaji wa umeme kwani iwapo huduma hiyo itakosekana
bado ni changamoto hata maeneo ya mijini “Anasema.
Anasema ni jambo jema kusikia kuwa hapa kwenu masuala ya mgawo wa
umeme kukatika itakuwa ni suala la
kusikia kwa wengine na huo ndio uzuri wa kutumia teknolojia ya umeme
wa Jua.
“Pamoja na hayo lakini niwahamasishe wananchi wa hapa mpale kutumia
vizuri uwepo wa nishati hiyo kwa
kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kuanzisha viwanda vidogo
vidogo na miradi itakayoweza kuwaingizia fedha ili kujikwamua
kiuchumi”Anasema.
“Msiishie kupata mwanga tu bali tumieni pia fursa hii kuanzisha
biashara na miradi itakayowaingizia fedha kwani umeme huu unatosha
kuanzisha viwanda vidogo vidogo kama vinu vya kusagia nafaka ,mashine za
useremala na kutengeneza samani “Anasema.
Anasema kwa kufanya hivyo wananchi wa kijiji hicho watakuwa
wameendana
sambamba na mwamko mpya wa Tanzania
ya Viwanda ambao utafungua fursa kubwa za kiuchumi kwao.
Naibu Katibu huyo anasema kupitia huduma hiyo ni matumaini yake
huduma
za afya zitaboreka zaidi kijijini hapo
kwani wananchi wengi wa maeneo ya jirani watakwenda kupata matibabu kwao
kutokana na uwepo wa uhakika
wa kutibiwa muda wote kunakosababishwa na nishati ya umeme.
“Nawaombeni halmashauri pamoja na serikali ya kijiji kujipanga
kuhakikisha umeme unaotumika unalipiwa kadri inavyotakiwa kila mwezi
kwani haipendezi kuona nishati hiyo ipo lakini zahanati inakosa huduma
hiyo kwa kushindwa kilipia “Anasema.
“Lakini pia nikuombe Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe pamoja na
uongozi wa kijiji mjipange hata kwa
kutumia fedha mtakazookoa kutoka kwenye manunuzi ya mafuta ya taa na
gesi kwa ajili ya jokofu la madawa muweze kulipia umeme “Anasema.
“Serikali sasa kupitia wakala wa Nishati imezindua rasmi mpango wa
tatu wa kusambaza umeme maeneo ya
vijijini na tumeweka lengo la kufikia vijiji vyote ifikapo mwaka
2022.
Naye, Msimamizi Mkuu wa Mradi huo,Prosper Magali anasema shughuli
za
mradi huo zilianza rasmi Machi mwaka
2014 baada ya kutembelea kijiji hicho pamoja na vyengine vilivyopo
wilayani Korogwe.
Anasema licha ya kutembelea wilaya hiyo lakini pia walitembelea
maeneo
mengine Tanzania kutafuta vijiji na
maeneo yanayofaa kwa miradi ya uzalishaji mdogo wa umeme kwa kutumia
teknologia ya umeme wa Jua.
Aidha anaeleza waliamua kuanza mradi wa mfano katika kijiji hicho
baada ya kuwa kijiji bora kwa vigezo
walivyoweka vya kiuchumi, kijamii na kimakjazi ukilinganisha na
vyengine walivyotembelea.
“Shughuli ya mradi zilifuatiwa na zoezi la kufanya upembuzi
yakinifu,
Mpango wa kibiashara (Bussines Plan)
pamoja na makadirio ya kiufundi mambo ambayo yalitusaidia kuandaa
nyaraka za kuwasilisha kwa wafadhili na wawekezaji mbalimbali
“Anasema.
“Baada ya hapo mmwaka 2014 mwishoni, Taasisi ya Energy and
Environment
Partnership (EEP) Program yenye makao
yake makuu huko Pretoria nchini Afrika kusini inayopata ufadhili wa
Serikali za Finland, Uingereza na Austria kupitia mpango wake wa kutoa
ufadhili wa miradi ya nishati endelevu kwa nchi za kusini na mashariki
ya Africa kwa mtindo wa
ushindani “Anasema
“June 10 mwaka 2015 tuliweza kusaini makubaliano rasmi ya EEP ya
ufadhili wa miaka miwili wa mradi huu
uliokuwa na thamani ya Euro 263,000 ikiwa ni asilimia 63 ya gharama za
mradi “Anasema.
Anaongeza kuwa bado wanaendelea na zoezi la kutafuta fedha zaidi za
kutekeleza mradi huo lakini kwa bahati
nzuri baada ya mazungumzo ya muda mfupi, Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya
Maendeleo ya Mitaji (United Nations Capital Development Fund ya
UNCDF).
Anaeleza kufuatia mazungumzo hayo taasisi hiyo ilikubali kutoa asilimia 22 ya gharama za mradi USD 124,000 na walitiliana saini ya makubaliano ya ufadhili wa fedha hizo Novemba mwaka 2015. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments:
Post a Comment