Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, akiangalia magazeti yanayozalishwa na Kampuni ya Mwananchi, alipotembelea kampuni hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Na
Shamimu Nyaki-WHUSM.
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel
amevishauri vyombo vya habari
kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kujua lugha sahihi
ya Kiswahili wakati wanapofikisha ujumbe wa kwa
jamii.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati
alipofanya ziara katika Kampuni ya
Magazeti ya Mwananchi (MCL) ambapo ameeleza kuwa Baraza la Kiswahili
lipo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza
Lugha ya Kiswahili hivyo vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika matumizi
sahihi ya Kiswahili.
“Vyombo vya habari mna nguvu kubwa kwa jamii na
mnafuatiliwa na watu wengi hivyo mnapaswa kujua matumizi sahihi ya lugha ya
Kiswahili katika uandishi,utangazaji pamoja na matumizi mengine katika
kuwasiliana na hadhira yenu,”alisema Prof. Elisante.
Aidha, ameongeza kuwa ni wajibu kwa wadau wa
habari kusoma vizuri na kuelewa Sheria
ya Huduma za Habari na kutambua mambo muhimu yaliyoanishwa katika Sheria hiyo
ikiwemo kuwa na Mikataba,Bima ya Afya na Bodi na Mfuko wa Habari utakaowawezesha
kupata ufadhili wa kusoma.
Hata hivyo ameipongeza Kampuni ya Mwanachi kwa
kuwa na Kitengo cha lugha ya Kiswahili na maktaba nzuri ya kuhifadhi magazeti
yote ambayo yameshasomwa na kuvishauri vyombo vingine kuwa na mfumo huo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
hiyo Bw. Francis Nanai amesema kuwa
Kampuni yake itaendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza majukumu yake
kwa manufaa ya nchi.


No comments:
Post a Comment