Pages

Tuesday, August 29, 2017

TAARIFA RASMI YA CUF KWA UMMA KUHUSU MASHAURI YALIYOPO MAHAKAMA KUU KESHO TAREHE 30/8/2017 KUANZIA SAA 3 ASUBUHI


TAARIFA KWA UMMA
KESHO mbele ya Majaji wawili wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Jaji Wilfred Ndyansobera na Mheshimiwa Jaji Lugano Mwandambo wataendelea kusikiliza mashauri yafuatayo;

MWANDAMBO . J
Shauri namba 479/2017 maombi ya Wabunge 8 na madiwani wawili kuhusu Zuio litasikilizwa na kupangiwa kutolewa Maamuzi. (Substantive issues raised by our MP’s and Councillor’s in the pleadings that may have to be determined by the court after perusal of evidence.)
NDYANSOBERA. J
1. Shauri Jipya la Madai Miscelleneous Civil Cause no. 69/2017 kati ya WAbunge 19 dhidi ya Lipumba na Seif Sharif Hamad litatajwa na Tayari Lipumba ameshapokea Summons ya kuitwa mahakama kesho. Viongozi hao wa Kiserikali kwa ujumla wao wanaiomba Mahakama; “Kumkataza Lipumba na wafuasi wake wanaodai kuwa na mamlaka kichama na au mtu mwingine yeyote yule kuwaita Wabunge, madiwani na au Viongozi wengine kwa lengo la kuwachukulia hatua za kinidhamu (Disciplinary Measure) mpaka pale Mashauri yaliyopo Mahakamani juu ya uhalali wa Uongozi wa Chama utakaposikilizwa na kutolewa Maamuzi. Viongozi hao wanaiomba Mahakama itoe nafuu (Relief) kwa kuwalinda na kuwaacha watekeleze Majukumu yao kwa mujibu wa sheria za nchi mpaka hapo Mgogoro huo utakapopatiwa ufumbuzi na kumalizika”
2. Shauri la Madai (Miscelleneous Civil Application No.28/2017) shauri hili ndilo lililoweka Zuio ya Ruzuku isitolewe. Litaletwa kesho kwa ajili ya Kusikilizwa na kutolewa maamuzi (Necessary Order) baaada ya shauri lake la msingi Namba 21/2017 kuondolewa Mahakamani tarehe 11/8/2017. Tayari shauri jingine Namba 68/2017 Limeshasajiliwa kureplace’ shauri namba 21/2017
3. Shauri la Madai (Civil Case No. 13/2017) linahusu uhalali wa wajumbe wa bodi ya wadhamini ya CUF iliyosajiliwa na RITA- Ally Salehe dhidi ya Lipumba na wenzake.
4. Shauri la Jinai namba 50/2017 (Contempt of Court Proceedings)-shauri hili dhidi ya Lipumba na wenzake, Emmy Hudson-RITA, Franscis Mutungi linahusiana na kughushi nyaraka na kutaka kuingilia mwenendo wa mashauri yaliyopo mahakamani.
5. Shauri namba madai namba 34/2017 maombi ya Lipumba na Thomas kuingizwa katika shauri namba 21/2017 linalohusu wizi wa fedha za Ruzuku.
TUJITOKEZE KSHUHUDIA HOJA ZA KISHERIA ZINAVYOWASILISHWA NA KILA MMOJA AMJULISHE MWENZAKE;
1. Waheshimiwa Wabunge wote makini watakuwepo.
2. Waheshimiwa Madiwani, wakiongozwa na Mhe Musa Kafana, Omary Kumbilamoto, na Ramadhani Kwangaya,
3. Waheshimiwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wakiongozwa na Bakari Kasubi,
4. Waheshimiwa Viongozi na Wanachama wa Matawi Dar es Salaam, Mhe Rashid Abdallah
5. Waheshimiwa Viongozi na Walinzi wote wa Chama [Blue Guards and White Guards]. Wakiongozwa na Trump’s Mkali, Juma Shaali, na Robert Mlwati.
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa leo Tarehe 29/8/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa
SALIM BIMAN
MKURUGENZI
+255 777 4141212 / +255 655 314112
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI
0715 062577 / 0767 062 577
maharagande@gmail.com

No comments:

Post a Comment