Pages

Thursday, August 10, 2017

WATUMISHI HOUSING COMPANY (WHC) YAFUNGUA MILANGO KWA WAFANYAKAZI KUNUNUA NYUMBA ZAKE KWA MIKOPO NAFUU YA MUDA MREFU

Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mfuko huo, kunza kuuza nyumba zake kwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali kwa mikopo nafuu ya muda mrefu. Kulia ni Afisa Mauzo na Mawasiliano wa WHC, Maryjane Makawia. 
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa WHC, Raphael Mwabuponde, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa WHC, Dk. Fred Msemwa na kulia ni Afisa Mauzo na Mawasiliano wa WHC, Maryjane Makawia. 
Afisa Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Irene Kasanda akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo, wakati akielezea namna wana Diaspora wanavyoweza kunufaika na mpango huo.
WATUMISHI Housing Company (WHC) ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulio anzishwa kwa lengo la kujenga na kuuza nyumba za bei nafuu kwa Watumishi wa umma kwa mikopo nafuu ya muda mrefu. 

Watumishi Housing Company (WHC) inapenda kuijulisha umma kwamba imefungua dirisha kwaajili ya kuuza nyumba zake kwa wafanyakazi wote. Hii inajumuisha wafanyakazi walio katika utumishi wa umma na wale ambao hawako katika utumishi wa umma lakini wanachangia katika mifuko ya pensheni. Wigo huu mdogo unakuja baada ya kuonekana watu wengi ukitoa watumishi wa umma wana shida ya makazi bora na ya kisasa ni wachangiaji katika mifuko ya pensheni ambayo ndiyo wamiliki wa Watumishi Housing, hivyo basi taasisi ikaona itoe nafasi kwa wachangiaji wengine wa mifuko ya pensheni kuweza kupata nyumba za kisasa, bora na za bei nafuu.


Kufuatia uamuzi huu, Watumish Hosing Company sasa itakua ikiwahudumia watumishi wa umma pamoja na wafanyakazi wengine walioko katika sekta binafsi. Uamuzi huu ni muendelezo wa juhudi za serikali na mifuko ya hifadhi ya jamii katika kuwawezesha wafanyakazi wote kuwa na makazi bora na kuwawezesha kiuchumi kupitia umiliki wa nyumba.


Watumishi Housing inapenda kuwakaribisha watanzania wote kwa ujumla kutuma maombi yao ya nyumba kwa kuchukua fomu katika tovuti ya  HYPERLINK "http://www.whctz.org" www.whctz.org au kwa kufika katika ofisi zilipo jengo la Golden Jubilee Towers ghorofa ya 4. Kwasasa tuna nyumba za kuuza zilizopo Bunju B, Gezaulole Kigamboni, Mkundi Morogoro, 


Mwanza Kisesa na Njedengwa Dodoma. Vilevile tunapenda kusisitiza kwamba watumishi wa umma watapewa kipaumbele katika kupata nyumba kwani wao ndio kipaumbele cha taasisi.


Watumishi Housing Company (WHC) ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja wenye jukumu la kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya watumishi wa umma. Jukumu lingine la WHC ni kusimamia dhamana ya uwekezaji nyumba (Real estate investment Trust- REIT) kupitia uwekezaji katika vipande. WHC inamilikiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii lakini baada ya muda si mrefu WHC itaweza kumilikiwa na kila mtanzania kupitia uwekezaji wa vipande.


Watumishi Housing tunashauri watumishi kununua nyumba tayari zilizojengwa na zilizo bora na za kisasa badala ya kununua ardhi na kuanza ujenzi. Kwakufanya hivi utakua unanunua nyumba ambayo tayari imeishajengwa kwa ubora na kisasa kwa bei nafuu kabisa vilevile utakua unaondokana na matatizo mengi sana yanayokuja na ujenzi kama kupoteza muda, gharama kubwa na n.k.

IMETOLEWA NA MKURUGENZI MTENDAJI
WATUMISHI HOUSING COMPANY

No comments:

Post a Comment