Marubani wawili wanaofanya kazi na shirika la ndege la serikali nchini Algeria wamefukuzwa kazi baada ya kumruhusu mtoto yatima mwenye umri wa miaka kumi kuendesha ndege ya abiria.
Mtandao wa Africa News unasema kuwa zoezi hilo lilifadhiliwa na kurekodiwa na runinga ya El Bilad TV, waliomuonyesha mtoto huyo akiwa amevaa sare za rubani akibofya vitufe katika chumba cha rubani.
- Ndege za China zazuia ndege ya Marekani
- Ndege zagongana nchini Canada
- Nusura ndege ya Canada igonge ndege nne uwanjani San Francisco
Haijulikani ni abiria wangapi walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Air Algerie kutoka mji wa Algiers hadi mji Setif.
Mtandao huo unasema kuwa rubani hao walifukuzwa tarehe 29 mwezi Julai huku uchunguzi zaidi ukifanywa kwa sababu kitendo hicho kilikiuka sheria za usafiri wa ndege.


No comments:
Post a Comment