Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akiagana na Viongozi mbali mbali wa Serikali na Vyama vya Siasa alipoondoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuelekea Nchini Jamhuri ya Cuba kwa ziara maalum. Meya na Manispaa ya Wilaya ya Magharibi “B” Mstahiki Maabadi Ali Maulid mwenye suti ya kijivu jivu akimtakia safari njema Balozi Seif katika ziara yake hiyo.(Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Ndugu Silima Haji Haji mwenye bashasha akimuaga Balozi Seif Ali Iddi aliyeambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi katika safari hiyo.
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
10/7/2017.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Zanzibar leo asubuhi kupitia Mjini Dar es Salaam kuelekea Nchini Jamuhuri ya Cuba kwa ziara Maalum.
Balozi Seif katika ziara hiyo ameondoka akifuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya wasaidizi wake kikazi.
Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar Balozi Seif aliagwa na baadhi ya Viongozi, Watendaji wa Serikali pamoja na Viongozi wa Vyama vya Kisiasa viliopo hapa Nchini.
Ziara ya Balozi Seif Nchini Jamuhuri ya Cuba pamoja na mambo mengine itajumuisha kutembelea Bunge la Nchi hiyo ambapo pia atapata wasaa wa kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chombo hicho cha juu cha kutunga Sheria.
Baadae Ballozi Seif atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Elimu, Naibu Waziri wa Afya pamja na kuona harakati za uzalishaji wa dawa katika Kiwanda cha Madawa cha Nchi hiyo sambamba na kufanya mazungumzo ya Ushirikiano wa pande hizo mbili.
Zaiara hiyo ya Balozi Seif imelenga kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu ulipo kati ya Cuba na Zanzibar hasa katika Sekta ya Afya na Elimu ambazo zimeleta mafungamano ya Nchi hizo rafiki Kihistoria.



No comments:
Post a Comment