TANGAZO


Friday, July 14, 2017

WATUMISHI 46 TEMESA WAPATIWA MAFUNZO YA UBAHARIA NA UNAHODHA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (aliyesimama), akiongea na watumishi, kutoka katika vituo 19 vya vivuko nchini vinavyosimamiwa na TEMESA. Watumishi hao walikua wakiagana na Dkt. Mgwatu baada ya kumaliza mafunzo yao yaliyotoleawa na Chuo cha Bahari cha jijini Dar es Salaam (DMI). (Picha zote na Theresia Mwami)  
Mkurugenzi wa Idara ya Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (aliesimama kushoto) akisoma taarifa ya mafunzo yaliyotolewa kwa baadhi ya Mabaharia na “Ferry Captains” 46 wa TEMESA kutoka katika vituo 19 vya Vivuko vinavyosimamiwa na wakala huo. 
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) waliomaliza mafuzo katika Chuo cha Bahari (DMI) wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TEMESA (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

Na Theresia Mwami
MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu, leo ameongea na watumishi mbalimbali kutoka kwenye vituo vya vivuko nchini vinavyosimamiwa na TEMESA waliohudhuria mafunzo katika Chuo Cha Ubaharia cha Dar es Salaam. 

Dkt. Mgwatu amewataka watumishi hao wa kada ya ubaharia pamoja na unahodha wa vivuko kwenda kuyatumia mafunzo hayo kwa vitendo na kuwa waadilifu na pia kutoa kauli nzuri kwa wateja wanaotumia huduma za TEMESA. 

Aidha Dkt. Mgwatu ameahidi kufuatilia kwa haraka suala la kuboresha mikataba ya ajira kwa watumishi wa muda ili wapate mikataba ya mwaka mmoja badala ya miezi mitatu kama ilivyo hivi sasa.

Awali katika taarifa yake Mkurugenzi wa Idara ya Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko TEMESA, Mhandisi Japhet Maselle, alisema kuwa watumishi 46 wamepatiwa mafunzo katika Chuo cha Ubaharia kwa muda wa wiki mbili na kuwa miongoni mwa kozi walizozisoma ni pamoja na “Refresher Course”, “Mandatory Course”, “Rating Course”pamoja na “Ship Security Course. 

Lengo hasa la mafunzo hayo ni kuboresha huduma za vivuko zinazosimamiwa na TEMESA nchini.

TEMESA ina jumla ya vivuko 29 katika vituo 19 pamoja na boti 4 ndogo zinazotumika nyakati za dharura.

No comments:

Post a Comment