Brafu inayoyeyuka nchini Uswisi imefichua miili miwili inayoaminiwa kuwa ya mtu na mkewe waliotoweka miaka 75 iliyopita.
Marcelin na Francine Dumoulin walitoweka wakati walienda kuchunga ng'ombe wao katika milima ya Alps mwaka 1942.
Watu hao walikuwa na watoto saba.
Mtoto wao wa mwisho wa kike ambaye sasa ana umri wa 79, anasema habri hizo zimemletea utulivu na anataka kuwafanyia maziko mema.
- Jiwe kubwa la barafu linalovutia watalii
- Barafu kubwa kumeguka Antarctica
- Space X kuwasafirisha watalii 2 mwezini 2018
"Tulitumia maisha yetu yote kuwatafuta," alisema Marceline Udry-Dumoulin.
Uchunguzi wa DNA unatarajiwa kufanywa.
Polisi wanasema kuwa miili hiyo iligunduliwa wiki iliyopita katika eneo la Tsanfleuron na mfanyakazi kutoka kampuni ya kuteleza kwa barafu ya Glacier 3000.
No comments:
Post a Comment