TANGAZO


Wednesday, July 12, 2017

WABUNGE KUTOKA UGANDA WATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi akipeana mkono na Kiongozi wa Msafara wa baadhi ya Wabunge kutoka Uganda Mhe. Cecilia Barbara wakati wa ziara yao katika Taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi akielezea jambo wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Bunge la Uganda waliotembelea Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Wabunge hao wametembelea Taasisi hiyo ili kujionea namna inavyofanya majukumu yake.
Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu akizungumza jambo mbele ya Wabunge kutoka Uganda walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Uganda Mhe. Cecilia Barbara na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi (katikati).  
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakifuatilia Maelezo kuhusu namna Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inavyofanya kazi wakati wa ziara yao katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wabunge kutoka Uganda wakiwa katika sehemu ya mapokezi ya kuingia Wodi ya Watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam. 
Msajili wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dkt. Zawadi Edward akielezea namna ambavyo wanawahudumia watoto wagonjwa wanaolazwa katika Taasisi hiyo wakati wa ziara ya Wabunge kutoka Uganda waliofika katika Taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wabunge kutoka Uganda walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa lengo la kujifunza leo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote Frank Shija - Maelezo)

No comments:

Post a Comment