Meneja wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Wilfred Mwingira akizungumza na wadadisi wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania yanayoendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Wadadisi wakijifunza kwa vitengo namna ya kutumia vifaa vya kielektroniki - tablets vitakavyotumika wakati wa Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo yanaendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.

Na Veronica Kazimoto, Dodoma
18 Julai, 2017.
UTAFITI wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili unatarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya wadadisi yanayoendelea kufanyika mkoani Dodoma Meneja wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Wilfred Mwingira amesema lengo kuu la utafiti huo ni kufuatilia viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza ili kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyotokea.
"Utafiti huu ni wa kitaifa na utafanyika Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyojitokeza kwenye viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza", amesema Mwingira.
Nae Mratibu wa utafiti huo Reiner Kiama amesema kuwa utafiti huu unafanyika ili kutathmini kama mpango unaleta manufaa yaliyokusudiwa katika ngazi ya kaya kwa kutumia viashiria kama vile elimu, afya, kazi na matumizi ya muda, shughuli za kaya zisizo za kilimo, mapato, mikopo, akiba na uhamishaji fedha.
Viashiria vingine ni shughuli za kilimo, makazi ya kaya na upatikanaji wa maji, matumizi na usalama wa chakula katika kaya, maamuzi katika kaya, ukatili kwa wanawake na matarajio ya vijana, mahusiano ya kaya na jamii pamoja na mtazamo wa kaya kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili utahusisha kaya takribani elfu saba (7,000) ambazo zilihojiwa katika utafiti wa awamu wa kwanza uliofanyika mwezi Juni, 2015.
No comments:
Post a Comment