Msanii wa Marekani Usher Raymond yuko ziarani nchini Tanzania akitembelea eneo la uhifadhi wa wanyama pori la Serengti National Park.
Bwana Raymond alichapisha baadhi ya picha akiwa na familia yake katika akaunti yake ya Twitter.
Alielezea hali ilivyo katika eneo hilo kama ya kufurahisha .
Ripoti za Usher Raymond kuzuru Tanzania zilisambaa kwa haraka nchini humo.
Watu wengine maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid David Becham, aliyekuwa mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho, mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin ni miongoni mwa wale waliozuri katika sehemu mbali mbali za kitalii nchini humo mwaka huu.
Vivutio vya kitalii nchini Tanzania kama vile mbunga ya uhifadhi wa wanyama pori ya Serengeti na mlima Kilimanjaro ni vivutio vinavyoongoza kwa utalii ambapo watu wengi maarufu wametembela.
No comments:
Post a Comment