TANGAZO


Thursday, July 13, 2017

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 13.07.2017 na Salim Kikeke

Pierre-Emerick Aubameyang

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAubameyang alijiunga na Borussia Dortmund kutoka St Etienne in 2014
Chelsea wameambiwa wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, kwa pauni milioni 60 baada ya Tianjin Quanjian ya China kusema haitaki tena kumsajili mchezaji huyo. (Daily Mail)
Borussia Dortmund huenda wakaamua kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, ambaye pia anasakwa na Everton, West Ham, Marseille na AC Milan. (Daily Mirror)
Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, amempigia simu meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na kumuambia hana mpango wa kuondoka Chelsea msimu huu. (Diario Gol)
Chelsea wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kwa pauni milioni 40 kwa mkataba wa miaka mitano. (RMC)
Meneja wa Chelsea anajiandaa kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwa pauni milioni 40. Matic amekuwa akifanya mazoezi peke yake na anataka kuungana na Jose Mourinho Old Trafford. (Daily Telegraph)
Barcelona wanataka kumsajili beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta baada ya kushindwa kumpata Hector Bellerin wa Arsenal. (Marca)
Chelsea watawazidi kete Juventus katika kumsajili beki wa kulia wa Real Madrid Danilo, 25, kwa pauni milioni 28. (Daily Mirror)
Mchezaji wa zamani wa Liverpool Danny Murphy amesema klabu hiyo inakaribia kukamilisha usajili wa Virgil van Dijk, 26, kutoka Southampton. (Sports360)
Tiemoue BakayokoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTiemoue Bakayoko
Arsenal wana uhakika dau la pauni milioni 45 litatosha kumsajili winga wa Monaco Thomas Lemar, 21. (Daily Mail)
Arsenal wanataka kumsajili kinda wa West Ham Domingos Quina, 17. (Sky Sports)
Roma wanataka kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 26. (Sky Italia)
Tottenham wamesema hawatoburuzwa na Manchester United na Manchester City kuhusu usajili wa Eric Dier na Kyle Walker, huku wakikaribia kumsajili beki Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 9. (Daily Telegraph)
Manchester United wana matumaini ya kukamilisha usajili wa winga wa Inter Milan Ivan Persic, 28, wiki ijayo. (Daily Star)
Manchester United sasa wataelekeza nguvu zao kumsajili kiungo wa Roma Radja Nainggolan, 29, kwa kutoa pauni milioni 40 baada ya Tottenham kukataa dau lolote kuhusu Eric Dier. (Daily Mail)
Ivan PerisicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIvan Perisic (kulia)
Leicester City huenda wakaondoa wachezaji sita waliosajiliwa msimu uliopita akiwemo Islam Slimani, 29, na Ahmed Musa, 24, pamoja na kiungo Nampalys Mendy, 25. (Daily Telegraph)
Middlesbrough wamewazidi kete Burnley na Watford katika kumsajili Britt Assombalonga, 24, kwa pauni milioni 14 kutoka Nottingham Forest. (Sun)
West Ham wanafikiria kupanda dau la tatu kumtaka Marco Arnautovic, 28, baada ya dau la pauni milioni 20 kukataliwa na Stoke City. (London Evening Standard)
Watford na Swansea zinamtaka kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah, 22. (Sun)
Real Madrid wamekata tamaa ya kumpata kipa wa Manchester United David de Gea, 26, msimu huu. (Daily Star)
Marko ArnautovicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMarko Arnautovic amechezea Stoke mechi 145
Manchester City wanakaribia kumsajili kiungo kutoka Brazil Douglas Luiz, 19, anayechezea Vasco da Gama. (ESPN)
Manchester City wanataka kupanda dau la pauni milioni 25 kumtaka beki wa Southampton Ryan Bertrand, 27, baada ya kumkosa Dani Alves aliyesaini PSG. (Daily Mail)
Stoke City watawazidi kete West Brom katika kumsajili beki wa Chelsea Kurt Zouma, 22 kwa mkopo. (Sun)
Fenerbahce ya Uturuki inataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, 23. (Fanatik)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza) : Uhamisho wa wachezaji Ulaya
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.

No comments:

Post a Comment