Rais wa shirikisho la kandanda nchini uhispania na mtoto wake wa kiume wamekamatwa kama sehemu ya uchunguzi wa polisi kuhusu ufisadi.
Angel MarĂa Villar Llona alikamatwa kwa kushukiwa kuvuja pesa.
Mr Villar, mchezaji wa zamani wa kimataifa ya Uhispania amekuwa rais wa shirikisho la kandanda la uhispania tangu mwaka 1988.
Mwanawe wa kiume Gorka ni kati ya watu waliokamywa wakati wa uavamizi uliofanya mara kadha maepema Jumanne.
Mahakama ya juu nchini Uhispania iliambia Reuters kuwa mmoja wa majaji wake na waendesha mashtaka wa masuala ya ufisadi wanaongoza uchunguzi huo.
Pia amehudumu katika baraza la la shirikisho la kandanda duniani Fifa kwa kipindi cha miaka 29 iliyopita lakini alitimuliwa na Fifa kwa kukataa kutoa ushirikiano kwenye uchunguzi kwa zoezi la kumtafuta mwandalizi wa kombe la dunia mwaka 2018 na 2022.
No comments:
Post a Comment