TANGAZO


Friday, July 14, 2017

Polisi wawili wa Israel wauawa karibu na eneo takatifu Jerusalem

Temple Mount/Haram al-Sharif (14/07/17)

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWashambuliaji hao waliandamwa hadi eneo la Temple Mount/Haram al-Sharif
Polisi wawili wa Israeli wamefariki baada ya Waisraeli watatu wa asili ya Kiarabu waliokuwa na silaha kuwamiminia risasi katika eneo la mji wa kale wa Jerusalem.
Maafisa wengine wa polisi waliwafuata washambuliaji hadi ndani ya eneo takatifu linalojulikana na Wayahudi kama Temple Mount na Waislamu kama Haram al-Sharif na kuwauwa wote watatu.
Afisa mwingine wa polisi alijeruhiwa.
Msikiti wa al-Aqsa, umefungwa na watu kuhamishwa.
Sala ya Ijumaa iliyopangiwa kufanyikia huko, imefutiliwa mbali kwa mara ya kwanza kwa miaka mingi.
Waziri wa usalama wa Israel, amesema kuwa, washambuliaji hao "walivuka mpaka".
Eneo hilo la kale la mji lipo katika maeneo ya Mashariki mwa Jerusalem, maeneo yaliyotwaliwa na Israel katika vita vikali vya mwaka 1967- hatua ambayo haitambuliwi na mataifa ya Dunia.
Kumekuwepo na msururu wa visa vya watu kuchomwa visu na wengine kukanyagwa au kugongwa kwa magari tangu mwaka 2015, walengwa sana wakiwa Waisraeli.
Mashambulio hayo hutekelezwa na Wapalestina au Waarabu Waisraeli.
Washambuliaji waliotekeleza mashambulio ya awali walikuwa wa asili ya Jordan.
Sgt Maj Hail Sattawi (left) and Sgt Maj Kamil ShananHaki miliki ya pichaWIZARA YA MAMBO YA NJE YA ISRAEL
Image captionSajini Meya Hail Sattawi (kushoto) na Sajini meya Kamil Shanan walifariki kutokana na majeraha ya risasi
Polisi wanasema wasahmbuliaji waliowashambulia polisi hao walikuwa na umri wa kati ya miaka 19 na 29 na walitoka mji wa Umm al-Fahm, kaskazini mwa Israel.
Shirika la usalama la Israel la Shin Bet limesema awali hawakuwa wanafahamika au kufuatiliwa na maafisa wa usalama.
Temple Mount/Haram al-Sharif graphic
Lions' Gate (14/07/17)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWaumini walishiriki sala ua Ijumaa nje ya eneo linalofahamika kama Lango la Simba baada ya msikiti kufungwa

No comments:

Post a Comment