Maryam Mirzakhani, mwanamke wa kwanza kushinda tuzo la hesabu la Fields Medal amefariki nchini Marekani.
Professor Mirzakhan mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni professor katika chuo cha Stanford, alikuwa akiugua ugonjwa wa Saratani ya matiti ambayo ilisambaa hadi kwa mifupa yake.
Alipewa jina mshindi wa Nobel ya hesabu. Tuzo la Fields Medal hutolewa baada ya kila miaka minne kwa kati wa wasomi wa hesabu wawili na wanne walio chini ya miaka 40.
Ilipewa Professor Mirzakhan mwaka 2014.
- Iran imemnyonga mwanasayansi kwa usaliti
- Iran 'yapuuzilia mbali' taarifa ya Trump kuhusu shambulio la Tehran
- Iran yakana watu waliokamatwa na Saudia ni wanajeshi wake
- Mshindi wa Oscar kutoka Iran amkosoa Trump
Rais wa Iran Hassan Rouhani alisema kuwa kifo cha Prof Mirzakhan kileta huzuni nyingi.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Mohammad Javad Zarif, alisem kuwa kifo chake kimewaletea majonzi watu wote nchini iran.
Prof Mirzakhani na mumewe ambaye ni mwanasayansi raia wa Czech, wana mtoto mmoja.
No comments:
Post a Comment