Maafisa sita wa serikali waliokuwa wametekwa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Shabab katika kaunti ya Lamu huko pwani ya Kenya wameokolewa kulingana na gazeti la The Star nchini humo.
Vyombo vya habari vimeripoti kwamba wapiganaji hao waliliteka na kulielekeza gari hilo lililokuwa na maafisa wa serikali katika eneo lisilojulikana.
Eneo hilo limekumbwa na mashambulio kadhaa katika kipindi cha majuma mawili yaliopita huku wapiganaji hao wakidaiwa kuwachinja watu tisa katika kijiji cha Jima wikendi iliopita.
Serikali ya Kenya imetuma jeshi katika eneo hilo, ambapo linatumia mashmbulio ya angani kulenga kambi za wapiganaji hao katika msitu wa boni, uliopo katika mpaka wa Kenya na Somalia ambapo wapiganaji hao wamekita kambi.
No comments:
Post a Comment