TANGAZO


Tuesday, July 18, 2017

KITUO CHA WAZEE NUNGE KIGAMBONI CHAPOKEA MSAADA WA VITU MBALIMBALI

Nabii, Samson Rolinga (wa kwanza kulia) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations lililopo Mbezi  Beach akizungumza jambo mara alipofika katika kituo cha Wazee cha Nunge kilichopo Kigamboni Dar es Salaam
Nabii, Samson Rolinga (katikati) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations lililopo Mbezi  Beach akiongoza maombi mara alipofika katika kituo hicho cha wazee hao na akiwa amefuatana na  waumini wake ambapo walitowa msaada mbalimbali na  kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kukata Keki kwa kusheherehekea  siku yake ya kuzaliwa na wazee wa Kituo cha Nunge Kigamboni
Waumini wa Kanisa la Omega wakisaidiana kuingiza ndani msaada hiyo. 
Mzee Vumilia Chambuso (kulia) akishukuru kwa niaba ya wazee hao akisema, napenda kuwashukuru kwa ujio wenu kwa kutenga muda wenu kwa kutukumbuka , Mungu awazidishiye na tunaomba msada wa umeme  kwani kunatatizo la umeme tunakuwa kiza kwa muda mrefu, Chamboso alisema kwa niaba ya sisi wazee tunawashukuru sana na Mungu awabariki na ifike siku moja mje muonane na uongozi mtuchukuwe tuje kupata Ibada kwa pamoja na tunauhitaji w dawa kwa baadhi ya wazee tunaugua maradhi mbalimbali, alimalizia kwa kuwashukuru na kuzidi kuwaombea kwa Mungu mafanikio tele.
Baadhi ya Keki.
Nabii, Samson Rolinga (katikati mwenye fulana nyeupe) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations akifurahia jambo alipokuwa katika picha ya pamoja na wazee hao.
Nabii, Samson Rolinga (katikati) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations akikata Keki pamoja na wazee hao na akiwa na baadhi ya waumini aki Sherehekea Siku yake ya kuzaliwa 
 Nabii, Samson Rolinga (kushoto) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations lililopo Mbezi  Beach akimlisha Mzee Vumilia Chambuso kipande cha Keki wakati alipofika katika kituo hicho
 Nabii, Samson Rolinga (kulia) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations lililopo Mbezi  Beach akimlisha kipande cha keki mmoja wa waumini alio ongozana nao 

 Nabii, Samson Rolinga (wakwanza kulia) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations lililopo Mbezi  Beach akiwapatia wazee hao baadhi ya msaada hiyo
 Nabii, Samson Rolinga (wakwanza kulia) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations lililopo Mbezi  Beach akiwapatia wazee hao baadhi ya msaada hiyo
 Nabii, Samson Rolinga (wa tatu kushoto) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations lililopo Mbezi  Beach akishirikiana na waumini kutowa Msaada Mbalimbali kwa Wazee  na watu wasiojiweza wa Kituo cha Nunge Kigamboni  na kusherehekea Siku yake ya kuzaliwa na wazee hao
 Nabii, Samson Rolinga (wa pili kushoto) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations lililopo Mbezi  Beach akishirikiana na waumini wake kutotoa Msaada Mbalimbali kwa kituo cha Wazee  na watu wasiojiweza Nunge Kigamboni 
 NaSamson Rolinga (wa pili kulia) wa Kanisa la Omega Ministrie Church Of  All Nations lililopo Mbezi  Beach atoa Msaada Mbalimbali kwa kituo cha Wazee  na watu wasiojiweza Nunge Kigamboni akishirikiana na waumini wake na kusherehekea Siku yake ya kuzaliwa 
 Nabii, Samson Rolinga (wa katikati) akizungumza jambo  baada ya kutowa msaada na kushukuru uongozi mzima wakituo hicho, alisema, tunamshukuru Mungu kutuwezesha kuiona siku ya leo na binafsi namshukuru kwa kuniwezesha kuion siku yaleo ambayo ndio siku yangu ya kuzaliwa. aleendelea kusem Rolinga.

Hayo aliyasema wakati alipofika katika Kituo cha Wazee waishio katika Kituo cha Nunge Kigambani Dar es Salaam, wakati alipofika katika Kituo hicho cha wazee Nunge, alipofika kuwajulia hali na kutowa msaada wavitu mbalimbali ikiwemo nguo, mchele, mafuta ya kula na pesa taslimu kwa kila mzee na familia. 

Nabii, Rolinga alisema, ninamuomb Mungu atuwezeshe n waumini wangu tuweze kusaidia kutatua changamoto zile tutakazo ziweza tukishirikiana na Uongozi tuweze saidiana na swala la umeme tutashirikiana na uongozi,

Naye Mwenyekiti wa Wazee hao,  Anthoni Kikongoti alishukuru kwa niaba ya wazee alisema, kwa ujio wenu Mungu awazidishiye na ninapingana na kauli ya wasemayo, eti wazee niwatu wanao subiri  kufa , alisema Kikongoti

Kauli hiyo ninapingana nayo kwani unaweza kufa kijana na sisi wazee tukabaki, hivyo naiasa jamii kutuona nasi ni watu kama watu wengine wanao hitaji mahitaji mengine na ikiwemo kula, kuvaa nakupata huduma stahiki.

Tuatowa shukrani zetu na kuomba wengine waone nasi tunawahitaji wao watulee kwani sisi wazee tumeluka chumvi nyingi na chakula bila chumvi utaona hakina radha yoyote  hivyo tunaomba mtulee sisi ni sawa na watoto wenu kwa hali yoyote tunawategemea ninyi.  

Mzee Vumilia Chmbuso nayeye alipata nafasi ya ya kuushukuru ujio wa   Nabii, Samson Rolinga aliyeongozana na waumini wake kutupatia msaada sisi wazee  nijambo la faraja kutukumbuka na Mungu azidi kuwabariki.
 Nabii, Samson Rolinga (kushoto aliye simama) akiongoza kuimba  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee hao akiwa na waumini wake
 Nabii, Samson Rolinga akiwapatia pesa taslimu baadhi ya wazee hao

No comments:

Post a Comment