TANGAZO


Thursday, July 13, 2017

Gazeti la Uingereza lauita mji wa Dar es Salaam ''Kijiji cha uvuvi''

Gazeti la Uingereza lakosolewa kwa kuuita mji wa Dar es Salaam ''Kijiji cha wavuvi''

Image captionGazeti la Uingereza lakosolewa kwa kuuita mji wa Dar es Salaam ''Kijiji cha wavuvi''
Watumiaji wa mtandao wa Twitter wanaendelea kulikosoa gazeti moja la Uingereza la Daily Mail kwa kuuita mji wa Dar es salaam ''kijiji cha wavuvi''.
Maneno hayo yalitumiwa katika habari kuhusu ziara ya klabu ya Everton nchini Tanzania.
Mtu mmoja aliitaja hatua hiyo kama utovu wa heshima na ya kibaguzi.
Hivi ndivyo lilivyoandika gazeti hilo la UingerezaHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionHivi ndivyo lilivyoandika gazeti hilo la Uingereza
Maneno hayo hatahivyo yameondolewa katika habari hiyo ambayo bado iko katika mtandao lakini bado yametumika katika maelezo ya picha, imesema.
''Mashabiki wa Bollasie wamejaa katika kijiji cha uvuvi mashariki mwa pwani ya taifa hilo'', yalisema maelezo hayo ya picha

No comments:

Post a Comment