Wayne Rooney (katikati), akipiga mpira na wachezaji wenzake wa Everton FC walipokuwa katika mpambano na timu ya Gor Mahia ya Kenya, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi, uliodhaminiwa na Sport Pesa.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wachezaji wa timu ya Everton FC wakisalimiana na viongozi mbalimbali kabla ya kuanza mpambano wao na Gor Mahia ya Kenya, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Wachezaji wa timu ya Everton FC wakisalimiana na wenzao wa Gor Mahia kabla ya kuanza kwa mpambano kati ya timu hizo, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Wachezaji wa akiba wa timu ya Everton FC wakiwa kwenye benchi leo wakati wa mpambano na timu ya Gor Mahia ya Kenya, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Everton FC wakipiga picha ya pamoja kabla ya mchezo kati ya timu hiyo na Gor Mahia ya Kenya, kuanza Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Gor Mahia ya Kenya wakipiga picha ya pamoja kabla ya mchezo kati ya timu hiyo na Everton FC ya Uingereza, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Mpira ukiwa umeanza Uwanja wa Taifa kati ya timu hizo mbili, ubao wa matangazo ulisomeka mabao Gor Mahia 0 na Everton 0.
Jonsol Kenny wa Everton (kushoto), akipambana na Mussa Mohamed wa Gor Mahia.
James Mc Cathy wa Everton (kushoto), akiwaniampira na Ochieng Welington wa Gor Mahia.
James Mc Cathy wa Everton (kushoto), akipambana na Ochieng Welington wa Gor Mahia.
Kijana akitolewa nje na askari baada ya kuvamia uwanja na kwenda kumkumbatia Wayne Rooney.
Hapa Everton ikiwa inaongoza kwa bao 1 lililofungwa na Wayne Rooney.
Wachezaji wa Gor Mahia wakifurahia baada ya kusawazisha bao hilo na kuwa bao 1-1 hadi mapunziko.
Ubao wa matokeo ukionesha Everton bao 1 na Gor Mahia bao 1.
Wayne Rooney akitoka nje ya Uwanja na wenzake baad ya kupulizwa kipenga cha mapumziko katika mchezo huo.
Mashabiki wakifuatilia mpira.
Mashabiki wakiwa wamejazana kwenye uwanja wakati wa mchezo huo.
Wachezaji wa Everton wakiingia uwanjani kuanza ngwe ya pili ya mchezo huo.
Meneja wa Everton, Coeman akielekea kwenye benchi la timu hiyo wakati wa kuanza ngwe ya pili ya mchezo huo
Wachezaji wa Gor Mahia wakiingia uwanjani kuanza ngwe ya pili ya mchezo huo
Mchezaji wa Everton, Tom Davies akimtoka Ochieng Welington wa Gor Mahia.
Dom Covert-Lewin wa Everton akipiga mpira mbele ya Wafua Innocent wa Gor Mahia.
Dom Covert-Lewin wa Everton akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kugongana na mchezaji wa Gor Mahia.
Hapa Everton ikiwa imejipatia bao la pili na hivyo ubao kusomeka Gor Mahia 1 na Everton 2.
Wachezaji wa Everton wakitoashukurani kwa Watanzania baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kutokana na kupata mapokezi mazuri.
Wayne Rooney (katikati), na wenzake wakitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezokati ya timu hizo.
Meneja wa Everton FC, Coeman akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Meneja wa Gor Mahia, Dylan Kerr akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment