TANGAZO


Monday, July 17, 2017

Ed Sheeran ashirikishwa katika Game of Thrones

Ed Sheeran on Instagram


Haki miliki ya pichaED SHEERAN/ INSTAGRAM

Mwanamuziki Ed Sheeran ameshirikishwa katika mwendelezo wa filamu za Game of Thrones - kama mwanajeshi.
Nyota huyo wa muziki aina ya Pop, anaimba na pia kuzungumza kwa muda mfupi katika makala ya sasa ya filamu hizo ambayo.
Sehemu ya kwanza ya makala ya sasa ilipeperushwa mapema leo.
Sehemu hiyo ambayo imepewa jina Dragonstone, ndiyo ya kwanza kwenye makala ya saba ya mwendelezo wa filamu hizo maarufu sana kutoka Marekani.
Uigizaji wa mwanamuziki huyo wa miaka 26 uliwagawanya mashabiki wake mtandaoni, baadhi wakifurahishwa naye na wengine kumkosoa.

GlastonburyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEd akiwa jukwaani katika tamasha ya Glastonbury mwezi uliopita

Mhusika ambaye Ed ameigiza jina lake halijatajwa.
Anaonekana akiimbia akiwa na watu wanaoota moto msituni.
Mhusika Arya Stark anayeigizwa na Maisie Williams anapopitia hapo akiwa kwenye farasi, anamwambia, "Ni wimbo mzuri huo, sijawahi kuusikia awali."
"Ni wimbo mpya," Sheeran anajibu.
Ed amefurahia kushirikishwa kwake kwa kupakia picha kadha katika akaunti yake mtandao wa Instagram.
Shabiki wake mmoja Kalynn alisema huo (kumuona Sheeran akiigiza) ulikuwa "wakati mwema zaidi kwangu maishani".
Ryan Kathleen Greene naye akaandika, "wakati mzuri sana kwamba nimekuwa hai".
Lakini wengine hawakufurahishwa, na Vann hata alipendekeza Arya Stark alifaa kumuua mhusika aliyeigizwa na Ed.
Sehemu hiyo ya Dragonstone itapeperushwa tena Sky Atlantic na Now TV leo usiku.
Makala yatakayofuata ya Game of Thrones yatakuwa ndiyo ya kwisho. Filamu hizo zimewepo tangu 2011.

No comments:

Post a Comment