Mshambuliaji wa kimataifa wa Uhispania, Diego Costa amepiga picha za video akifurahia likizo yake huku akiwa amevalia jezi ya Atletico Madrid.
- Katika picha hizo za video alizopakia kwenye mtandao wake wa Instagram, nyota huyo alivaa jezi ya timu yake hiyo ya zamani, huku akiandika ujumbe kwa mchezaji mwenzake Cesc Fabregas kuwa amkumbatie meneja wao Antonio Conte.
- Costa apewa muda zaidi kupumzika Chelsea
- Costa anaamini Chelsea hawamtaki
Mustakabali wa Costa bado haujawekwa sawa toka nyota huyo alipobainisha kuwa Conte alimwambia kuwa hahitajiki tena kwenye klabu hiyo.
Matokeo hayo yamemfanya Costa mwenye umri wa miaka 28 kuachwa katika kikosi cha Chelsea kilichoanza maandalizi ya msimu ujao huku kukiwa na matumaini ya kupata klabu mpya.
No comments:
Post a Comment