TANGAZO


Monday, July 17, 2017

BANK OF AFRICA YAKABIDHI RASMI MTAMBO WA UJENZI AINA YA GREDA KWA MTEJA WAKE

Naibu Mkurugenzi mtendaji wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Wasia Mushi akikabidhi mfano wa funguo kuashiria makabidhiano ya Greda kwa Mteja Bw. T Hitesh Vishram ambae ni Project Supervisor wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Limited, Katikati ni meneja wa masoko, Utafiti na maendeleo wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Muganyizi Bisheko.


BANK OF AFRICA hii leo imekabidhi rasmi mtambo wa ujenzi (Greda jipya aina ya JCB) lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300 kwa kampuni ya Dezo Civil Contactors Limited, kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo kandarasi ya ujenzi wa kuta kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi.

Makabidhiano ya mtambo huu ni sehemu ya mpango endelevu wa benki wa kununua na kukodisha mitambo (lease finance), ambayo inawawezesha wateja kujiongeza kiutendaji kwa kupata vifaa vya kisasa bila ya kulazimika kuwa na pesa taslimu za manunuzi ya vifaa hivyo.

Makubaliano haya ya ukodishaji wa mitambo yanaakisi katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano, utalii, madini, mafuta na gesi.

BANK OF AFRICA imebaini huu ni mpango ambao una tija kubwa kwa wajasiriamali wakubwa kwa wadogo, kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa biashara zao ambao utaongeza uzalishaji na faida kubwa. Mteja kupitia mpango huu anapewa fursa pana ya kufanya chaguo lake bila kikwazo chochote na bila ya uhitaji wa amana ya awali au dhamana nyingine. Marejesho ni malipo ya ukodishaji ya kila mwezi na mteja ana uwezo wa kuchagua kua mmiliki wa mali husika pindi ifikapo mwisho wa mkataba wa ukodishaji.

Benki humsaidia mteja kuhakiki chombo anachotaka kuingianacho mkataba kama kina ubora ili kuweza kuinua uchumi wake na uchumi wataifa kwa ujumla.

BANK OF AFRICA ilianza shughuli zake Juni mwaka 2007, baada ya kuinunua Benki ya Euroafrican ambayo ilianza kazi Tanzania kutokea September 1995.

BANK OF AFRICA inafanya kazi katika mtandao wa benki za biashara katika nchi 18 zikiwamo nchi za Benin, Burkina Faso, Burundi, Cote d”ivoire, Djibouti, DRC, Ethiopia, France, Ghana, Kenya, Madagascar, Mali, Niger, Rwanda, Senegal, Tanzania, Togo na Uganda.

Kundi la Group BANK OF AFRICA lina makao makuu yake jijini Dakar, Senegal ikiwa na mtandao wa watu 500 wale wanaotoa huduma na sapoti kwa ofisi. Kuanzia mwaka 2010, Group BANK OF AFRICA ilimilikiwa kwa wingi wa hisa BMCE Bank, ambayo ni benki ya pili kwa ukubwa nchini Morocco.

BMCE Bank huleta mikakati mizito ya msaada wa uendeshaji katika kuunga mkono shughuli za BANK OF AFRICA Group, vilevile na muunganiko na ukaribu wa kufikia masoko ya kimataifa kutokana na uwepo wake katika nchi za Ulaya na Asia.

No comments:

Post a Comment