Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Kijana Khamis Mgaya Juma aliyelazwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmmoja baada ya kushambuliwa na Vijana Mtoni Kidatu Jumanne ya Tarehe 11 Julai 2017. Wa kwanza kutoka kulia anayemsaidia Mgonjwa Khamis ni Baba Mzazi Mzee Mgaya Juma na kulia ya Balozi Seif ni Muuguzi wa Zamu ya Wagonjwa wa Wodi ya Mifupa Biubwa Hassan Juma.(Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)
Majeruhi Khamis Mgaya Juma aliyelala kitandani akimuelezea Balozi Seif Mkasa uliomkubwa wakati aliposhambuliwa kwa mapanga na Vijana wasiopungua Saba Eneo la Mtoni Kidatu na kumjeruhi sehemu za Kichwa, Mikono na Miguu. Balozi Seif akiwaagiza wauguzi kuzingatia maadili yao ili kupunguza malalamiko yanayotolewa na wagonjwa wakati akimfariji Kijana Khamis Mgaya aliyejruhiwa kwa mapanga Jumanne iliyopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya (kulia), Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dr. Mustafa Garu.
Balozi Seif akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyomshirikisha Waziri wa Elimu Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dr. Mustafa Garu.
Balozi Seif wa Pili kutoka Kulia akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya aliyeko upende wa Kulia yake. Wa kwanza kutoka Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma, wa kwanza kutoka Kushoto ni Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana Setandar Kumar na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dr. Mustafa Garu.
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
17/7/2017.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameliagiza Jeshi la Polisi Nchini kuwasaka na kuwatia mikononi mara moja Vijana Waliohusika na kitendo cha kinyama cha kumshambulia kwa Mapanja Utingo wa Dala dala ya bara bara ya Mtoni Kidatu - Darajani Kijana Khamis Mgaya Juma mnamo Tarehe 11 Julai 2017.
Alisema kitendo hicho ambacho hakikubaliki kibinaadamu hata kisheria kinastahiki kulaaniwa na Jamii nzima na Serikali Kuu kupitia vyombo vya Ulinzi haitakubali kuona tabia kama hiyo inaendelea kushuhudiwa Mitaani.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati alipofika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kumkagua na kumfariji Kijana Khamis Mgaya Juma mwenye umri wa Miaka 24 aliyepata mtihani huo akiwa kazini mwake Hapo Mtoni Kidatu Wilaya ya Magharibi “A”.
Khamis Mgaya licha ya kupata majeraha makubwa sehemu za Kichwa, Miguu pamoja na mikono yote miwili baada ya kushambuliwa kwa silaha za jadi za Mapanga na Vijana zaidi ya Saba hivi sasa anaendelea kupata nafuu licha ya kubakiwa na maumivu katika mwili wake.
Balozi Seif alisema polisi licha ya doria wanazoendelea kuzifanya sehemu mbali mbali Nchini lakini bado kuna haja ya kuafuatilia nyendo za watu wanaoripotiwa kwao kuhusika na vitendo viovu ikiwemo ujambazi.
Alisema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa inaweza ikatoa fursa kwa wananchi kuwa na amani pamoja na utulivu wa kuendelea na harakati zao za Kimaisha bila ya wasi wasi wowote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimtakia matibabu mema Kijana Khamis Mgaya Juma na kumuomba aendelee kuwa na subira wakati huu wa maumivu wakati Serikali kupitia vyombo vya Ulinzi vitahakikisha wale wote waliohusika na tatizo lililomkubwa wanaonja mkono wa sheria.
Balozi Seif halkadhalika waliwakumbusha Madaktari na Wauguzi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili bila ya kujali wanao muhudumikia ana wadhifa au cheo gani.
Alisema baadhi ya Madaktari hasa wauguzi wamekuwa wakiripotiwa kuhusika na vitendo vya kunyanyasa wagonjwa mambo ambayo yako nje ya maadili yao ya kazi.
Balozi Seif alisema Serikali imetoa msukumo wa kuwapatia Wananchi matibabu bure lakini bado wapo baadhi ya watu dhana hiyo wamekuwa wakiiwekea vikwazo visivyo na msingi kwa kuwasumbuwa Wananchi hao.
Mapema Majeruhi Khamis Mgaya Juma alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba alipatwa na kasa huo Jumanne ya Tarehe 11 Julai baada ya Mmoja wa abiria aliowachukuwa kwenye Gari yake kukataa kulipa Nauli.
Kijana Khamis alisema licha ya kumsamehe Kijana huyo baada ya kubishana muda wote wa safari lakini Abiria huyo aliamua kutafuta Vijana wenzake na kupanga njama ya kutaka kumfanyia hujuma wakati akiendelea na harakati zake za kazi.
Alisema Vijana hao walilazimika kukodi gari kumfuatilia Utingo huyo na hatimae kufanikiwa kumavia wakati wakishusha Abiria katika maeneo ya Mtoni kidatu wakitokea Mjini Darajani.
Khamis alielezea masikitiko yake pale alipoomba msaada kwa wasamaria waliopo katika na eneo hilo la tukio wakati akiendelea kushambuliwa kwa mapanga lakini wazee waliokuwa karibu ya tukio hilo walihamasisha Vijana hao kuendelea kumpiga.
Kijana Khamis Mgaya Juma alimshukuru msaramia Mmoja aliyekuwa akipita eneo hilo alipofanya juhudi za kutafuta gari na kumpelekea Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja bila ya msaada wowote wa watu waliokuwa karibu na eneo hilo.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo yao yaliyohudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} Dr. Mustafa Garu Balozi wa India Bwana Sandeep alisisitiza umuhimu wa kuanzishwa miradi mipya itakayostawisha Jamii kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa pande hizo mbili.
Balozi Sandeep alisema India hivi sasa imejipanga kuona miradi iliyoahidi kuitekeleza kwa Tanzania ya huduma za Maji safi na Salama upande wa Zanzibar pamoja na vifaa kwa ajili ya Vituo vya kazi za amali inakamilika kwa wakati.
Alisema uimarishaji wa Vituo vya Amali utatoa nafasi kubwa kwa Vijana kupata mafunzo ya vitendo yatakayowajengea uwezo mpana wa kujipatia ajira badala ya kusubiri kutoka Serikali Kuu.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliishukuru Serikali ya India kwa uamuzi wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzani kwa ujumla katika kusaidia miradi ya Maendeleo.
Balozi Seif alisema Miradi ya Maji safi na Salama Visiwani Zanzibar pamoja na Msaada wa Vifaa kwa ajili ya Vituo vya Amali Nchini ni masuala ya msingi kwa wakati huu katika kuimarisha ustawi wa Wananchi.
Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Balozi huyo wa India Nchini Tanzani kwamba Zanzibar bado inaendelea kuhitaji vifaa vya Kilimo kama Matrekta kwa lengo la kusaidia nguvu za Wakulima katika sekta ya kilimo.
Balozi Seif alieleza kwamba asilimia kubwa ya Wananchi wa Zanzibar wanaendelea kutegemea Sekta ya Kilimo katoka kujipatia riziki zao na kupunguza ukali wa maisha.
No comments:
Post a Comment