Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu wakijadili kwa umakini na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt.
Mpoki Ulisubisya wakati wakiongea na waandishi wa habari(Hawapo kwenye picha)
juu ya taarifa ya kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi. Hasma Juma katika hospitali ya
Temeke jijini Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakari Kambi akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari (Hawapo kwenye picha) wakatati wa uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi Hasma Juma uliofanyika mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
Waandishi wa habari wa vituo tofauti wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za kuibiwa mtoto mmoja wa Bi Hasma Juma uliowasilishwa leo na mwenyekiti wa kamati Dkt. Charles Majige ambae pia ni Daktari bingwa wa Magonjwa yakina mama , uliofanyika leo mapema katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akijibu maswali yaliyoulizwa na Waandishi
wa Habari juu ya tuhuma za kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi.Hasma Juma katika
Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa familia ya Bi. Hasma Juma Jordan Jaddah akifuatilia kwa umakini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (kushoto), wakati akisisitiza juu ya taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa kamati ya Uchunguzi Dkt. Charles Majige juu ya kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi. Hasma Juma.
Na WAMJW, Dar es Salaam
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea taarifa kutoka kwa tume huru aliyoiunda
ili kuchunguza malalamiko ya Bi. Asma Juma kuhusu kuibiwa mtoto mmoja kati ya
mapacha wawili katika hospitali ya Rufaa ya Temeke Dar es Salaam.
Akipokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa tume hiyo Daktari
bingwa wa magonjwa ya kinamama Dkt. Charles Majige Waziri Ummy amesema kuwa Bi. Asma Juma(29) hakuwa
na watoto mapacha kama ilivyodaiwa na mlalamikaji huyo kutokana na kipimo cha
Utra sound kukosea katika uchukuaji picha ya mtoto akiwa tumboni.
“Nimepokea taarifa kutoka kwa tume
huru niliyoiunda hivi karibuni na imethibitisha kuwa Bi. Asma Juma hakuwa na
watoto mapacha ila uchukuaji mbaya wa picha ya mtoto aliyekuwa tumboni uliofanywa
katika zahanati ya Huruma ukatoa matokeo hayo” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
wanafamilia ya Bi. Asma wanatakiwa kumfariji ndugu yao na sio kumkumbushia
jambo hili mara kwa mara kwani litamharibu kisaikolojia na kushindwa kutekeleza
wajiu wake kwa mtoto kama mama mzazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati
hiyo Dkt. Charles Majige Amesema kuwa Bi. Asma aliamini hivyo kwa sababu
Hospitali ya temeke hawakumchukua vipimo vya picha bali walitumia taarifa ya
vipimo vya awali.
Aidha Dkt. Majige Amesema kuwa tume
hiyo imebaini kuwa Bi. Asma hakuibiwa mtoto na alikua hana mapacha kwa sababu
uzito wake ulikua sio wa kubeba watoto wawili na katika chumba cha upasuaji
kulikua na wataalamu 6 kutoka vitengo mbalimbali.
Kwa upande wake mwakilishi wa Familia
ya Bi. Asma Juma Jordan Jaddah amesema kuwa anaishukuru Serikali kupitia Wizara
ya Afya kufatilia jambo hilo kwa ukaribu na kupata ukweli wa malalamiko yao na
wameikubali taarifa hiyo.
“Tunaipongeza tume hiyo chini ya
Wizara ya Afya na tunashukuru kwa msaada wao mwanzo mpaka mwisho na kutupatioa
majibu ya kuridhisha nasi tutakuwa bega kwa bega katika kumfariji ndugu yetu
kwa jambo hili lilitokea” alisema Bw. Jaddah.
Mbali na hayo Waziri Ummy amempongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa maagizo ya
kila mtoto wa kike atakaepata ujauzito shuleni asirudi shuleni ila aendelee na
masomo mengine ya ujuzi.

No comments:
Post a Comment