aziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Serengeti Boys pamoja na viongozi wa timu hiyo katika hafla ya kuwakaribisha baada ya kurejea kutoka katika michuano ya AFCON nchini Gabon jana Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Lorietha Laurence - WHUSM)
Wachezaji wa timu ya vijana chini ya miaka 17 “Serengeti Boys” wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) katika hafla ya kuwakaribisha baada ya kurejea kutoka katika michuano ya AFCON nchini Gabon jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimpa mkono wa kumkaribisha nyumbani mchezaji wa Serengeti Boys Bw. Abdul Sulemani
(kushoto) katika hafla ya kuwapokea wachezaji hao waliorejea nchini kutoka
katika michuano ya AFCON nchini Gabon jana Jijini Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe ameipongeza timu ya vijana chini ya miaka 17 “Serengeti Boys” kwa hatua
nzuri waliyofikia katika kiwango cha
Soka la Afrika kwa kushika nafasi ya pili katika kundi B walilokuwa wanacheza
wakati wa michuano ya AFCON iliyomaliziki hivi karibuni Mjini Gabon.
Pongezi hizo zimetolewa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa
hafla ya kuipokea timu hiyo katika viwanja vya ndege vya Kimataifa vya Mwalimu
Nyerere ambapo Waziri Mwakyembe aliwataka walimu na wachezaji hao
kuendelea kujiandaa kwa ajili ya mashindano mengine yaliyo mbele yao.
“Nimefurahi kwa hatua mliyoifikia na watanzani wote wanawapongeza
kwa kuwa mmeshindana kwa uwezo wenu na kuirudisha Tanzania katika ramani ya soka baada ya kukaa nje ya michezo ya
AFCON kwa takribani miaka 30 alisema” Mhe Mwakyembe.
Aidha aliongeza kuwa hapo walipofika wao ni mashujaa na Serikali
inaahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa vipaji hivyo vinaendelezwa kwa ajili ya ngazi
nyingine za kisoka.
Naye Kocha wa Serengeti Boys Kim Paulsen ameiomba Serikali na
wadau wa michezo nchini kuendelea kuisadia timu hiyo katika maandalizi mbalimbali ili
kuipa motisha zaidi katika kufanikisha ndoto ya Tanzania katika mchezo wa soka.
Kwa upande wake kapteni wa timu ya Serengeti Boys Bw. Dickson
Job amewashukuru watanzania kwa
mchango mkubwa walioutoa kwao katika
maandalizi mpaka hapo walipofikia ingawa hawakufanikiwa kurudi na ushindi.
“Mchezo una matokeo matatu kushinda, kushindwa au kutoka sare
ingawa hatukutarajia kushindwa kwa kuwa tulitamani sana kurudi na ushindi kama ambavyo tuliwaahidi watanzania ila mwaka
huu bahati haikuwa yetu ila tunaahidi kuendeleza mapambano katika hatua zijazo” alisema Bw. Job.
Timu ya Serengeti Boys imerejea nyumbani baada ya kumalizika
kwa michuano ya AFCON ambapo watapumzika na kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa
na michuano inayofuata ya chini ya miaka 20 inayounda timu ya Ngorongoro
Heroes.



No comments:
Post a Comment