Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.(Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango)
Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
Ujumbe wa Tanzania na Uganda ukishuhudia tukio la utiwaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi, akihutubia baada ya kutia saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Bw. George Masaju (kulia) na Mwanasheria wa Uganda Bw. Milliam Byaruhanga (kushoto), wakionesha nakala za Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania, Profesa Paramagamba Kabudi (kulia) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Bi. Irene Muloni (kushoto) wakionesha Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, baada ya kuusaini, tukio lililofanyika leo katika Hoteli ya Serena, Kampala, Uganda.
Hafla ya kutia saini Mkataba huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Kampala, Uganda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali, Wakurugenzi na Viongozi wa taasisi mbalimbali zinazohusika katika mradi huo.
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Tanga Tanzania, unatarajia kusisimua uchumi wa nchi hizo mbili na katika mchakato wa ujenzi wake zaidi ya watu 10,000 wanatarajiwa kunufaika na ajira.
Hivi Karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliuelezea mradi huo kuwa ni mkubwa kwakuwa Uganda imegundua shehena kubwa ya mafuta katika eneo la Hoima kiasi cha mapipa bilioni 6 na laki 5 na kwamba Tanzania inatarajia pia kupata mafuta kule ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambayo yatapitishwa katika bomba hilo hilo.

No comments:
Post a Comment