Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitabasamu wakati Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi wakiwa katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo nchini yamefanyika Kitaifa katika Chuo cha Ushirika, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Sehemu ya Wafanyakazi waliofika kwenye Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Na Nuru Juma, Husna Saidi - Maelezo
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aahidi nyongeza ya kawaida kwa
mishahara na kuwapandisha madaraja wafanyakazi wanaostahili.
Rais Magufuli ametoa
ahadi hiyo leo alipokuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chuo Cha Ushirika, Moshi
Mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Magufuli alisema
Serikali ilisitisha upandishaji wa vyeo na mishahara kutokana na kuwepo na
watumishi hewa na walioghushi vyeti lakini baada ya kuondolewa Serikali
itahakikisha inashughulikia maslahi ya wafanyakazi.
“Watumishi 9932
walikuwa na vyeti feki,watumishi hewa walikuwa 19706 hivyo kama Serikali
ingeongeza mishahara inamaana watumishi hawa pia wangefaidika na pesa ambazo
hawakustahili kuzipata”, alisema Dkt. Magufuli.
Aidha aliwataka
waajiri kuheshimu na kutoa mikataba ya kazi na kutowanyanyasa wafanya kazi wao
na wafanyakazi kuomba kazi kulingana na elimu zao na waache tabia ya kughushi
vyeti.
Aliongeza kuwa Serikali
itashughulikia mfumuko wa bei za bidhaa na kuhakikisha viwanda vingi vitajengwa
sehemu mbalimbali nchini ili kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu wa TUCTA Dkt. Yahya Msigwa ameipongeza Serikali kwa kutekeleza
ahadi zake na kuopngeza kuwa hiyo ni ishara tosha kuwa Serikali inayodhamira ya
dhati ya kuwajali wananchi wake wakiwemo wafanyakazi.
Ameongeza kuwa wanayo
imani kubwa kwa Serikali kuwa itatekeleza ahadi yake ya kufanyia maboresho ya
maslahi ya umma kama ambavyo umeonyesha nia njema ya kutekeleza ahadi zake.
Alizitaja baadhi ya
ahadi zilizotekelezwa kuwa ni pamoja, kupiga vita rushwa na ufisadi, kuondoa
watumishi hewa, Serikali kuhamia Dodoma, ujenzi wa miundombinu ya reli, vita
dhidi ya dawa za kulevya pamoja na ununuzi wa ndege.
“Ni imani yetu kuwa
ahadi hii ya kuboresha maslahi kwa Watumishi wa Umma itatekelezwa kwa wakati kwani
tayari umekwisha ondoa mambo yaliyokuwa yanakwamisha zoezi hilo,” alisema Dkt.
Msigwa.
Wakati huohuo Katibu
Mkuu huyo ameiomba Serikali kuharakisha kubuni namna ambavyo wafanyakazi
watanufaika na Mifuko ya Jamii na wanaodai mapato yao kusikilizwa kesi zao kwa
wakati.
Maadhimisho hayo
yameuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Makamu wa Rais Mama
Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai, Naibu Spika Tulia Ackson, Mawaziri Jenister Mhagama na Angella Kairuki,
Profesa Jumanne Maghembe na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na
baadhi ya Wabunge.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Uchumi wa Viwanda Vizingatie Haki, Maslahi na Heshima ya Mfanyakazi”.




No comments:
Post a Comment