Na
Husna Saidi & Nuru Juma- Maelezo, Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa inampango wakuunda kikosi kazi
cha kupitia changamoto zinazowakabili Wanafunzi wanaomaliza kidato cha Sita kutojiunga
na mafunzo yaJeshi kama sheria ya Jeshi la kujengaTaifa inavyotaka.
Hayo
yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Hussein Mwinyi
alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na George Huruma Mkuchika Mbunge
wa jimbo la Newala Mjini.
Dkt.
Mwinyi alisema kuwa Sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa ya mwaka 1964 imeweka ulazima
wa vijana wa Tanzania wanaomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria, hatahivyo mwaka 1994 Serikali iliyasitisha
kwa muda mafunzo hayo na kuyarejesha tena mwaka 2013 na yanaendelea hadi sasa.
“Takwimu
zilizopo zinaonyesha kupungua kwa idadi ya vijana wanaojiunga na mafunzo hayo muhimu
ya jeshi la kujenga Taifa hali hii imesababishwa na changamoto mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kugongana kwa tarehe za kuanza mafunzo ya vijana kwa mujibu wa sheria
na kufunguliwa kwa vyuo mbalimbali hapa nchini ambapo mihula ya mafunzo huanza”,
alisema Dkt. Mwinyi.
Aidha
alisema hali hiyo imewafanya vijana wengi walioteuliwa kujiunga na vyuo kukosa nafasi
ya kujiunga na mafunzo ya JKT kwamujibu wa sheria na changamoto nyingine ni ubovu
wa miundombinu, rasilimali watu na pamoja na fedha, hatahivyo Serikali inaendelea
na juhudi za kupata suluhu ya changamoto hizo.
Dkt.
Mwinyi aliongeza kuwa mwaka 2014 vijana waliohitimu kidato cha sita walikuwa
41,968 na kati yao waliojiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa walikuwa
31,692 ambao ni sawa na asilimia 75.5.
Aidha
mwaka 2015 kulikuwa na wahitimu 40,753 na waliojiunga ni 19,990 sawa na asilimia
48.8 huku mwaka 2016 wahitimu kidato cha sita walikuwa 63,623 waliojiunga na Jeshi
ni 14,747 sawa na asilimia 23.2.
Zoezi
la kuwachagua vijana hao kujiunga na mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa halina vigezo
maalum kwani kila kijana aliyemaliza kidato cha sita anasifa ya kujiunga na mafunzo
hayo.

No comments:
Post a Comment