Na Daudi
Manongi-Maelezo, Dodoma
SERIKALI kupitia
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa itaendelea
kuhamasisha Halmshauri zote nchini
kununua viuadudu vya kibailojia kwa ajili ya kuua viluilui vya mbu waenezao
Malaria vinavyotengenezwa na kiwanda cha Biotec product cha Kibaha.
Hayo yamesemwa leo
Bungeni na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe.Dk Hamis Kigwangala wakati
akijibu swali la Mbunge wa Gando Mhe.Othman Omar Haji.
“Viuadudu hivi
bimeanza kutengenezwa kuanzia mwezi Desemba 2016 na kwa sasa uhamasishaji huu
unaendelea na endapo viuadudu ivi
vitatumiwa vizuri vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha maambukizi
ya Malaria nchini”,Alisema Mhe.Kigwangalla.
Aidha amesema
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ushirikiano na Serikali ya Cuba
imeendelea kushirikiana katika mambo mengi ikiwemo pamoja na Sekta ya Afya
tangu mwaka 1986 mkataba uliposainiwa kati ya Serikali hizi mbili.
Kupitia mkataba huo
Serikali ya Tanzania imekuwa ikipokea madaktari bingwa kutoka Cuba ambao
wamekuwa wakifanya kazi katika Hospitali za Muhimbili,Hospitali ya Rufaa ya
Kanda Mbeya , Hospitali Tumbi na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
Mbali na hayo amesema
kuwa Madaktari hao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za kibingwa kwa wananchi
na kuwajengea uwezo madaktari wanaofanya nao kazi katika Hospitali hizo.
Aidha kwa kushirikiana
na kampuni ya Labiofarm ya Cuba,Serikali imeweza kujenga kiwanda cha
kutengeneza viuadudu ivyo na Serikali ya Cuba imeleta wataalamu.
Kiwanda icho cha
Biotec cha kibaha kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 2.5 za viuatilifu
vya kuua viluilui vya mbu waenezao
Malaria kwa mwaka.

No comments:
Post a Comment